إعدادات العرض
“Hakika mtafuata njia za walio kuwa kabla yenu, hatua kwa hatua, na dhiraa kwa dhiraa,
“Hakika mtafuata njia za walio kuwa kabla yenu, hatua kwa hatua, na dhiraa kwa dhiraa,
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khuduriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: “Hakika mtafuata njia za walio kuwa kabla yenu, hatua kwa hatua, na dhiraa kwa dhiraa, hata wakiingia kwenye pango la mburukenge, mtawafuata.” Tukasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, unakusudia Mayahudi na Wakristo? Akasema: “Kwa hiyo ni nani?”
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Kurdî Português සිංහල دری অসমীয়া ไทย Tiếng Việt አማርኛ Svenska Кыргызча Yorùbá ગુજરાતી नेपाली Oromoo മലയാളം Română Nederlands Soomaali پښتو తెలుగు Kinyarwanda ಕನ್ನಡ Malagasyالشرح
Anaeleza rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, jinsi hali ya baadhi ya watu wa Umma wake watakavyokuwa baada ya zama zake, ambako ni kufuata njia ya Mayahudi na Wakristo katika imani, matendo, desturi na mila zao, kufuata kwa undani sana, inchi kwa inchi, na dhiraa kwa dhiraa, hata wakiingia katika tundu la mburukenge, nao wataingia nyuma yao.فوائد الحديث
Hii ni alama miongoni mwa alama za utume wake, kwani alilieleza hilo kabla halijatokea, na limetokea kama alivyoeleza.
Katazo la Waislamu kuwaiga makafiri, iwe katika imani zao, ibada, sherehe, au nguo zao maalum kwa ajili yao.
Kufafanua mambo ya yasiyoonekana kwa mifano ya vitu vyenye kuonekana, hii ni katika mbinu za kufundishia katika Uislamu.
Mburukenge: Ni mnyama ambaye shimo lake lina giza kupindukia na lina harufu mabaya. Ni mtambaazi ambaye hupatikana kwa wingi jangwani, na sababu ya kufananisha na shimo la mburukenge ni wembamba wake sana na ubaya wake. Hata hivyo, kwa sababu ya kufuata mienendo yao, na kufuata kwao njia zao, laiti wangeingia kwenye wembamba huu mbaya namna hiyo, basi wangelikubaliana nao! Tunamuomba Mwenyezi Mungu Msaada!.
التصنيفات
Kujifananisha kulikokatazwa