Mcheni na Allah Mola wenu Mlezi, na salini swala zenu tano, na fungeni mwezi wenu, na tekelezeni zaka zenu, na mtiini mwenye mamlaka kwenu, (Mkiyafanya haya) mtaingia pepo ya Mola wenu

Mcheni na Allah Mola wenu Mlezi, na salini swala zenu tano, na fungeni mwezi wenu, na tekelezeni zaka zenu, na mtiini mwenye mamlaka kwenu, (Mkiyafanya haya) mtaingia pepo ya Mola wenu

Kutoka kwa Abuu Umama radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akihutubu katika Hija ya kuaga akasema: "Mcheni na Allah Mola wenu Mlezi, na salini swala zenu tano, na fungeni mwezi wenu, na tekelezeni zaka zenu, na mtiini mwenye mamlaka kwenu, (Mkiyafanya haya) mtaingia pepo ya Mola wenu".

[Sahihi]

الشرح

Alihutubia Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ya Arafa, katika Hija ya kuaga, mwaka wa kumi hijiria (tangu kuhama kutoka Makka) na Hija hiyo iliitwa hivyo kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwaaga watu ndani yake, Na akawaamrisha watu wote wamuogope Mola wao Mlezi kwa kutekeleza amri zake na kuepuka makatazo yake. Na wasali swala tano alizozifaradhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu usiku na mchana. Na wafunge mwezi wa ramadhani. Na wawape zaka ya mali wastahiki wake na wasizifanyie ubahili. Na wawatii aliowafanya Mwenyezi Mungu kuwa viongozi juu yao, pasipokuwa na kumuasi Mwenyezi Mungu, atakayefanya mambo haya yaliyotajwa basi malipo yake ni kuingia peponi.

فوائد الحديث

Matendo haya ni katika sababu za kuingia peponi.

التصنيفات

Ubora na fadhila za matendo mema.