إعدادات العرض
Shikamana na kusujudu kwa wingi kwa ajili ya Allah, kwani hakika wewe huta sujudu kwa ajili ya Allah isipokuwa Allah atakupandisha kwa sijida hiyo daraja, na atakufutia kwa sijida hiyo makosa
Shikamana na kusujudu kwa wingi kwa ajili ya Allah, kwani hakika wewe huta sujudu kwa ajili ya Allah isipokuwa Allah atakupandisha kwa sijida hiyo daraja, na atakufutia kwa sijida hiyo makosa
Kutoka kwa Ma'adan Bin Abi Twalha Alya'mary amesema: Nilikutana na Thauban muachwa huru wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake nikasema: 'Niambie matendo nitakayo yafanya (iwe sababu kwa Allah) kuniingiza Peponi' au alisema, nikasema: matendo mazuri yanayopendeka zaidi kwa Allah, akanyamaza, kisha nikamuuliza akanyamaza, kisha nikamuuliza kwa mara ya tatu akasema: Nilimuuliza hayo Mtume wa Allah rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Shikamana na kusujudu kwa wingi kwa ajili ya Allah, kwani hakika wewe huta sujudu kwa ajili ya Allah isipokuwa Allah atakupandisha kwa sijida hiyo daraja, na atakufutia kwa sijida hiyo makosa" Akasema Maadan: Kisha nikakutana na Abuudardaa nikamuuliza, akanambia mfano wa hayo alionambia Thauban.
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt සිංහල Hausa Kurdî Português தமிழ் دری অসমীয়া አማርኛ Svenska ไทย Yorùbá Кыргызча ગુજરાતી नेपाली Română മലയാളം Nederlands Oromoo తెలుగు پښتو Soomaali Kinyarwanda Malagasyالشرح
Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu matendo yanayopelekea kuingia Peponi au kuhusu matendo yanayopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu? Basi rehema na amani za Allah ziwe juu yake akamwambia muulizaji: Dumu na sijida kwa wingi, kwani kila unapomsujudia Mwenyezi Mungu anakunyanyua daraja kwayo, na anakusamehe dhambi kwa sababu ya sijida hiyo.فوائد الحديث
Muislamu amehimizwa kuswali swala za faradhi na za sunna, kwakuwa zinakusanya ndani yake kusujudu.
Kumebainishwa uelewa wa Maswahaba na elimu yao kuwa pepo haipatikani -baada ya huruma ya Mwenyezi Mungu- isipokuwa kwa matendo.
Kusujudu ndani ya swala ni katika sababu kubwa za kunyanyuliwa daraja, na kusamehewa madhambi.
التصنيفات
Fadhila za Swala.