Ikiwa kama utakuwa kama ulivyosema, basi ni kana kwamba unawalisha majivu ya moto (dhambi wanazozipata ni kama mtu anayekula majivu ya moto), Na bado anaendelea kuwa pamoja nawe msaidizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu dhidi yao, madam bado uko katika hali hiyo

Ikiwa kama utakuwa kama ulivyosema, basi ni kana kwamba unawalisha majivu ya moto (dhambi wanazozipata ni kama mtu anayekula majivu ya moto), Na bado anaendelea kuwa pamoja nawe msaidizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu dhidi yao, madam bado uko katika hali hiyo

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba mtu mmoja alisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mimi nina ndugu wa karibu, ninawaunga lakini wao wananitenga, ninawafanyia wema lakini wao wanatendea ubaya, na ninakuwa mpole kwao lakini wao wananifanyia ujeuri, Basi akasema: "Ikiwa kama utakuwa kama ulivyosema, basi ni kana kwamba unawalisha majivu ya moto (dhambi wanazozipata ni kama mtu anayekula majivu ya moto), Na bado anaendelea kuwa pamoja nawe msaidizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu dhidi yao, madam bado uko katika hali hiyo".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Ameeleza Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa mtu mmoja alisema kumwambia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Hakika mimi nina ndugu wa karibu ninawaunga lakini wao wananitenga, na ninawafanyia wema na wao wananifanyia ubaya, na ninawafanyia upole na wao wananifanyia ujeuri" Basi nifanye nini? Akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Ikiwa kama utakuwa kama ulivyosema, basi ni kana kwamba unawalisha majivu ya moto (dhambi wanazozipata ni kama mtu anayekula majivu ya moto), Na bado anaendelea kuwa pamoja nawe msaidizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu dhidi yao, madam bado uko katika hali hiyo" Yaani msaidizi, atakunusuru Mwenyezi Mungu hata kama ni baadae. "Na neno majivu": Yaani majivu ya moto, unawapakia wao wenyewe katika midomo yao, Nalo ni fumbo kuwa huyu mtu atanusurika dhidi yao, na si muungaji wa udugu wake yule anaye mlipa aliyemuunga, lakini muungaji wa kweli ni yule ambaye ukikatwa ukoo wake anauunga, na huyu ndiye muungaji wa kweli, ni wajibu kwa mwanadamu asubiri na ataraji malipo juu ya maudhi ya ndugu zake wa karibu na jirani yake na jamaa zake na wengineo, hatoacha kuendelea kuwa na msaidizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu yao, na yeye ndiye mwenye kupata faida na wao ndio weye kupata hasara.

التصنيفات

Ubora wa kuunga udugu.