Kumtukana Muislamu ni ufasiki (kutoka nje ya mipaka), na kupigana naye ni ukafiri

Kumtukana Muislamu ni ufasiki (kutoka nje ya mipaka), na kupigana naye ni ukafiri

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kumtukana Muislamu ni ufasiki (kutoka nje ya mipaka), na kupigana naye ni ukafiri."

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemkataza muislamu kumshutumu na kumtukana ndugu yake muislamu, nakuwa hilo ni katika ufasiki ambao ni kutoka nje ya utiifu wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, nakuwa muislamu kukabiliana na ndugu yake muislamu ni katika matendo ya ukafiri, lakini ni ukafiri mdogo.

فوائد الحديث

Ulazima wa kuheshimu heshima ya muislamu na damu yake.

Ukubwa wa hatima ya kumtukana muislamu pasina haki; mwenye kutukana pasina haki ni muovu.

Kumtukana muislamu na kupigana naye kunadhoofisha imani na kuipunguza.

Baadhi ya matendo huitwa ukafiri; hata yasipofika katika ukafiri mkubwa wenye kumtoa mtu katika Uislamu.

Makusudio ya ukafiri hapa ni ukafiri mdogo usiomtoa mtu katika Uislamu kwa makubaliano ya watu wa sunna; kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu ameuthibitisha udugu wa kiimani kwa waumini wakati wa kupigana kwao, akasema Mtukufu: "Na ikiwa makundi mawili ya waumini yatapigana basi wasuluhisheni baina yao" mpaka katika kauli yake: "Hakika waumini wote ni ndugu".

التصنيفات

Mambo mazuri na Adabu- Heshima., Tabia mbovu.