Hana swala yeyote ambaye hakusoma sura kifunguzi cha kitabu (suratul faatiha)

Hana swala yeyote ambaye hakusoma sura kifunguzi cha kitabu (suratul faatiha)

Kutoka kwa Ubaada bin Swaamit -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume -Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Hana swala yeyote ambaye hakusoma sura kifunguzi cha kitabu (suratul faatiha)".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa sala haikubaliki isipokuwa kwa kusoma suratul Fatiha, nayo ni nguzo miongoni mwa nguzo za swala, katika kila rakaa.

فوائد الحديث

Haikubaliki kusoma sura isiyokuwa suratul Fatiha ikiwa ana uwezo wa kuisoma.

Kuharibika kwa rakaa ambayo haikusomwa ndani yake suratul fatiha, kwa mwenye kufanya kusudi na mjinga na aliyesahau; kwa sababu ni nguzo, na nguzo huwa hazidondoki kwa hali yoyote ile.

Kisoma cha Suratul Fatiha kinaondoka kwa maamuma anapomkuta imam karukuu.

التصنيفات

Nguzo za swala, Nguzo za swala