Atakayejikatia haki ya muislamu kwa mkono wake wa kulia, basi Mwenyezi Mungu atakuwa kamuwajibishia moto, na kamharamishia pepo" Bwana mmoja akamuuliza: Hata kikiwa kitu kidogo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Hata kikiwa kijiti cha mswaki wa Araki

Atakayejikatia haki ya muislamu kwa mkono wake wa kulia, basi Mwenyezi Mungu atakuwa kamuwajibishia moto, na kamharamishia pepo" Bwana mmoja akamuuliza: Hata kikiwa kitu kidogo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Hata kikiwa kijiti cha mswaki wa Araki

Kutoka kwa Abuu Umama Iyaasi bin Tha'laba Al-Haarithy radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayejikatia haki ya muislamu kwa mkono wake wa kulia, basi Mwenyezi Mungu atakuwa kamuwajibishia moto, na kamharamishia pepo" Bwana mmoja akamuuliza: Hata kikiwa kitu kidogo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Hata kikiwa kijiti cha mswaki wa Araki".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuapa uongo kwa jina la Mwenyezi Mungu ili kujikatia haki ya muislamu, kwani malipo ya hilo ni kustahiki moto, na kunyimwa pepo, nalo ni katika madhambi makubwa. Bwana mmoja akasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu: Hata kikiwa kilichoapiwa ni kitu kidogo? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hata kikiwa ni kijiti cha mswaki unaochukuliwa kutoka katika mti wa Araki.

فوائد الحديث

Tahadhari ya kuchukua haki za watu wengine, na pupa ya kuzitekeleza kwa wenye nazo vyovyote vile zitakavyokuwa ndogo, nakwamba hukumu ya hakimu yeyote kuhukumu kimakosa hakuhalalishi haki isiyokuwa yake.

Amesema Nawawi: Uzito wa uharamu wa haki za waislamu, nakuwa hakuna tofauti baina ya haki ndogo na nyingi; kwa mujibu wa kauli yake rehema na amani ziwe juu yake : "Hata kikiwa kijiti cha mswaki".

Amesema Nawawi: Adhabu hii ni kwa yule atakayejikatia haki ya muislamu na akafa kabla ya kufanya toba, ama atakayetubia akajuta kwa kitendo chake na akairejesha haki kwa mwenye nayo, na akajivua nayo, na akaazimia kutorudia, basi dhambi itakuwa imemuondokea.

Amesema: Kumhusisha muislamu kwa sababu wao ndio wanaosemeshwa na wote wenye kuamiliana katika sheria, si kwamba asiyekuwa muislamu yuko kinyume na hivyo, bali hukumu yake ndiyo hukumu yake katika hilo.

Amesema Nawawi: Uongo ni kueleza kitu kinyume na jinsi kilivyo, kwa makusudi au kwa kusahau, sawa sawa kuelezea kwa wakati uliopita au ujao.

التصنيفات

Unyang'anyi