Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu, kisha akaja katika swala ya Ijumaa akasikiliza na akanyamaza atasamehewa yale yaliyoko kati ya Ijumaa yake hiyo na Ijumaa ijayo na ziada ya siku tatu

Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu, kisha akaja katika swala ya Ijumaa akasikiliza na akanyamaza atasamehewa yale yaliyoko kati ya Ijumaa yake hiyo na Ijumaa ijayo na ziada ya siku tatu

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu, kisha akaja katika swala ya Ijumaa akasikiliza na akanyamaza atasamehewa yale yaliyoko kati ya Ijumaa yake hiyo na Ijumaa ijayo na ziada ya siku tatu, na atakayegusa kijiwe basi atakuwa kafanya mchezo"

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye kutawadha na akaufanya vyema udhu wake kwa kukamilisha nguzo zake na kufuata Sunna zake na adabu zake, kisha akaswali swala ya Ijumaa na akanyamaza na kumsikiliza mhutubu, na akanyamaza pasina kuleta mazungumzo yasiyofaa; Basi Mwenyezi Mungu atamsamehe madhambi yake madogo kwa muda wa siku kumi, kuanzia sala ya Ijumaa hadi Ijumaa ya pili na ziada ya siku tatu, kwa sababu jambo jema huzidishwa mara kumi. Kisha rehema na amani ziwe juu yake akatahadharisha juu ya moyo kutojali mawaidha yanayosemwa katika hotuba, na kuchezea viungo kwa kugusa kokoto na aina nyinginezo za upuuzi na kujishughulisha, hayo yote ni katika aina ya mchezo na kujishughulisha kusikofaa, kwani mwenye kufanya hivyo atakuwa kafanya mchezo, na atakayefanya mchezo atakuwa hana fungu kamili katika ujira wa swala ya Ijumaa.

فوائد الحديث

Himizo la kutawadha na kuukamilisha kikamilifu, na kushikamana na sala ya Ijumaa.

Fadhila za swala ya Ijumaa.

Ulazima wa kunyamaza kwa ajili ya hotuba ya Ijumaa, na kutojishughulisha kwa mazungumza au kinginecho.

Iwapo mtu atafanya mchezo wakati wa hotuba Swala ya Ijumaa itakuwa sahihi na haitomlazimu kurudia swala ya faradhi, isipokuwa itakuwa na upungufu wa malipo.

التصنيفات

Ubora wa Swala ya Ijumaa.