Dua hairejeshwi (inayoombwa) baina ya adhana na kukimiwa swala

Dua hairejeshwi (inayoombwa) baina ya adhana na kukimiwa swala

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Dua hairejeshwi (inayoombwa) baina ya adhana na kukimiwa swala".

[Sahihi]

الشرح

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake fadhila za dua baina ya adhana na ikama, nakuwa dua hiyo hairejeshwi na inanafasi kubwa ya kujibiwa, basi muombeni Mwenyezi Mungu ndani ya wakati huu.

فوائد الحديث

Fadhila za wakati huu kwa ajili kuomba dua.

Atakapojipamba muombaji kwa adabu za kuomba dua, na akatafuta mahala pake na nyakati zake bora, na akajiepusha na kumuasi Mwenyezi Mungu, na akachukua tahahadhari ya kutotumbukia katika mambo yasiyofaa na yenye kutatiza, na akamdhania vizuri Mwenyezi Mungu: Basi ni rahisi sana kujibiwa, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Amesema Al-Munawi kuhusu kujibiwa dua: Yaani: Baada ya kukusanya sharti za dua na nguzo zake na adabu zake, ikiwa kitapelea kitu chochote basi asilaumu ila nafsi yake.

Ni sunna kuomba dua: Ima zijibiwe haraka dua zake, au aepushiwe katika shari mfano wake, au atunziwe Akhera; na hii ni kulingana na hekima ya Mwenyezi Mungu na huruma yake.

التصنيفات

Sababu za Kujibiwa Dua.