إعدادات العرض
Hakika ungesema maneno manne, mara tatu, kama ungeyapima kwa uliyo yasema toka siku ya leo yangeyazidi uzito
Hakika ungesema maneno manne, mara tatu, kama ungeyapima kwa uliyo yasema toka siku ya leo yangeyazidi uzito
Imenukuliwa kutoka kwa Juwairia mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku moja alitoka kwake asubuhi pindi alipo sali sala ya asubuhi, na yeye akiwa katika sehemu yake ya kusalia, kisha akarudi baada ya kuingia wakati wa dhuha, naye akiwa amekaa, akasema: "Bado upo kwenye hali yako niliyo kuacha nayo?" Akasema: "Ndio", Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika ungesema maneno manne, mara tatu, kama ungeyapima kwa uliyo yasema toka siku ya leo yangeyazidi uzito: Sub-haana llahi Wabihamdihi, Adada khalqihi, Waridhwaa nafsihi, Wazinata Arshihi, Wamidaada kalimaatihi" (Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema ni zake, kwa idadi ya viumbe vyake, na ridhaa ya nafsi yake, na uzito wa Arshi yake, na wino wa maneno yake)
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Hausa Kurdî Tiếng Việt অসমীয়া Nederlands አማርኛ සිංහල ไทยالشرح
Alitoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa mkewe mama wa waumini Juwairia radhi za Allah ziwe juu yake mwanzo wa asubuhi aliposwali swala ya Alfajiri, na Juwairia akiwa kakaa mahali aliposwalia, kisha akarejea baada ya mchana kufika kati kati wakati wa dhuha, naye akiwa bado kakaa katika mahali pake, akasema: Hivi bado uko katika hali niliyokuacha nayo? Akasema: Ndio, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hakika nimesema baada yako maneno manne, na nimeyakiriri mara tatu, lau yangelinganishwa kulingana na malipo na yale uliyoyasema kwa muda wote uliokaa hapa basi yangeliyazidi: "Ametakasika Mwenyezi Mungu" na kutakasika kwake kutokana na mapungufu, "na sifa njema ni zake" kiasi ambacho ana sifa nzuri ambazo amewaongoza kwazo, "idadi kubwa ya viumbe wake" ambazo hakuna awezaye kujua idadi yake isipokuwa Mwenyezi Mungu, "na ridhaa ya nafsi yake" kwa kiasi kinachomridhisha kutoka kwa wale aliowaridhia Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake nalo ni jambo lisiloelezeka, "na uzito wa Arshi yake" ambacho ndicho kiumbe kikubwa na kizito zaidi, "na wino wa maneno yake" na maneno ya Mwenyezi Mungu hayadhibitiki kwa idadi na wala hayamaliziki; na hii inakusanya migawanyiko yote mitatu na inazienea; kwani wino wa maneno yake Mtukufu hauna mwisho wa kiwango chake, wala sifa yake, wala idadi yake, lakini makusudio yake: Ni kupita kipimo katika wingi; kwa sababu yeye ametaja mengi mwanzoni yanayoweza kuhesabika miongoni mwa viumbe, kisha akapanda juu kwa makubwa zaidi katika hayo na akayaelezea kwa neno ridhaa ya nafsi yake, kisha uzito wa kiumbe kikubwa nacho ni Arshi; vya kwanza ni vya kuhesabika na kiwango maalumu, na vya pili ni kwa sifa na namna maalumu, na vya tatu ni kwa ukubwa na uzito.فوائد الحديث
Kumebainishwa fadhila za maneno haya, na himizo la kuyasema.
Dhikri zinazidiana ubora, ziko baadhi yake ni bora kuliko zingine.
Amesema Nawawi kuhusu kauli yake "Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema ni zake kwa wino wa maneno yake": Na makusudio yake ni kupita kiasi katika wingi; kwa sababu ametaja mwanzo yanayoweza kudhitibiwa na idadi kubwa miongoni mwa idadi ya viumbe vyake, kisha uzito wa Arshi, kisha akapanda juu zaidi kwa viumbe vikubwa kuliko hivyo, na akavielezea kwa hili, yaani yale yasiyodhitiwa na idadi kama ambavyo hayahesabiki.
Amesema bin Qayyim: Hakika kinaingia katika moyo wa mwenye kumtaja Mwenyezi Mungu wakati anaposema: Sub-haanallaahi wabihamdihi, adada khalqihi...mpaka mwisho wake katika kumjua kwake na kumtakasa kwake kwa kiasi hiki kilichotajwa cha idadi ni jambo kubwa kuliko kinachokita katika moyo wa msemaji, anaposema: "Sub-haanallaah" pekee.
Tumeelekezwa katika maneno machache yanayokusanya maana pana, yanayobeba matamshi kidogo, na yanalipwa kwayo fadhila na thawabu kubwa.
التصنيفات
Nyiradi za Asubuhi na Jioni.