"Ondosha tatizo, ewe Mola wa watu, na ponya kwani wewe ndiye mponyaji, hakuna ponyo ila ponyo lako, ponyo lisiloacha ugonjwa

"Ondosha tatizo, ewe Mola wa watu, na ponya kwani wewe ndiye mponyaji, hakuna ponyo ila ponyo lako, ponyo lisiloacha ugonjwa

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapomuendea mgonjwa basi anamuombea dua, anasema "Ondosha tatizo, ewe Mola wa watu, na ponya kwani wewe ndiye mponyaji, hakuna ponyo ila ponyo lako, ponyo lisiloacha ugonjwa".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapomtembelea mgonjwa anamuombea dua kwa kusema: Ewe Mwenyezi Mungu "Ondoa" ondosha "ugumu" na ukali wa maradhi, "Ewe Mola wa watu" na Muumba wao na Mlezi wao, "na ponya" maradhi haya "wewe" Mtukufu "Ndiye mponyaji" na ninaomba kupitia jina lako Mponyaji, "hakuna ponyo" linaloweza kupatikana kwa mgonjwa "isipokuwa ponyo lako" na afya yako, "ponyo" la moja kwa moja "lisiloacha" na kubakisha na kuacha "ugonjwa" na maradhi mengine.

فوائد الحديث

Mponyaji ni Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na daktari na dawa hivyo vyote ni sababu, havinufaishi wala havidhuru isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Kumtembelea mgonjwa ni katika haki zilizoko baina ya waislamu, nayo kwa familia inakuwa ni haki zaidi.

Himizo kwa mwenye kumtembelea mgonjwa amuombee dua hii yenye baraka na iliyonukuliwa kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Miongoni mwa muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kujitibu kwa kisomo (cha Ruqya) ya kisheria kwa Qur'ani na dua nzuri, alikuwa rehema na amani ziwe juu yake akijisomea mwenyewe anapougua, na vile vile alikuwa akimsomea yeyote mwenye kuhisi maumivu katika familia yake na watu wengine pia.

Amesema bin Hajari: Na imewatatiza baadhi ya watu dua ya kumuombea mgonjwa kupona hali yakuwa katika maradhi kuna kufutiwa madhambi na kupata thawabu kama zilivyokuja hadithi kwa wingi kuhusu hilo, na jawabu la hilo: Nikuwa dua ni ibada, na wala haiondoi thawabu na kufutiwa makosa; kwa sababu hayo hupatikana mwanzoni mwa ugonjwa na pale mtu anaposubiri juu ya maradhi, na muombaji anakuwa kati ya neema mbili: Ima apate lengo lake, au apewe badala kwa kuletewa manufaa au kuzuiliwa madhara, na yote hayo ni kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

التصنيفات

Ruq'ya ya Kisheria., Adabu za kumtembelea mgonjwa.