Alikuwa Mtume wa Allah -rehema na amani ziwe juu yake ni mkarimu kuliko watu wote, na alikuwa mkarimu zaidi anapokuwa katika mwezi wa Ramadhani pindi anapokutana na Jibrili

Alikuwa Mtume wa Allah -rehema na amani ziwe juu yake ni mkarimu kuliko watu wote, na alikuwa mkarimu zaidi anapokuwa katika mwezi wa Ramadhani pindi anapokutana na Jibrili

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alikuwa Mtume wa Allah -rehema na amani ziwe juu yake ni mkarimu kuliko watu wote, na alikuwa mkarimu zaidi anapokuwa katika mwezi wa Ramadhani pindi anapokutana na Jibrili, na alikuwa akikutana naye katika kila usiku wa Ramadhani akimsomesha Qur'ani, basi hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na Amani ziwe juu yake- ni mkarimu zaidi kwa mambo ya kheri kuliko hata upepo uliotumwa.

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa mkarimu zaidi kuliko watu wote katika mwezi wa Ramadhani, kiasi ambacho alikuwa akitoa kinachostahiki kumpa anayestahiki, na sababu ya kuzidisha ukarimu huu ni mambo mawili: La kwanza: Ni kukutana kwake na Jibril amani iwe juu yake. Na jambo jingine: Ni kuirejea Qur'ani, nayo ni kuisoma pasina kutazama mahali ilipoandikwa. Kwa hiyo Jibril, amani iwe juu yake, alisoma naye kila kilichoteremshwa katika Qur'ani, na Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake ni mkarimu zaidi, na ni mtenda kheri zaidi, na ni mwepesi wa kunufaisha viumbe kuliko upepo mzuri anaoutuma Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mvua na rehema.

فوائد الحديث

Kumebainishwa ukarimu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na upana wa ukarimu wake hasa katika mwezi wa Ramadhani, kwani ni mwezi wa utiifu na misimu ya matendo mema.

Himizo la ukarimu kila wakati, na ni sunna kuzidisha zaidi katika mwezi wa Ramadhani.

Kukithirisha utoaji wa misaada na ihsani na kusoma Qur'ani katika mwezi wa Ramadhani.

Katika sababu za kuihifadhi elimu ni kujisomea pamoja na wanafunzi wengine na wanachuoni.

التصنيفات

Ramadhani., Ukarimu wake Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake: