Atakapotoa matumizi mtu kwa familia yake kwa kutaraji malipo, basi hiyo kwake ni sadaka

Atakapotoa matumizi mtu kwa familia yake kwa kutaraji malipo, basi hiyo kwake ni sadaka

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapotoa matumizi mtu kwa familia yake kwa kutaraji malipo, basi hiyo kwake ni sadaka".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakapotoa mtu matumizi kwa familia yake, wale anaolazimika kuwahudumia kama mke wake na watoto wake na wengineo huku akijikurubisha kwa Allah Mtukufu kwa hilo, na akitaraji malipo kwake kwa yale anayowahudumia basi atakuwa na malipo ya sadaka.

فوائد الحديث

Hupatikana malipo na thawabu kwa kuihudumia familia.

Muumini hutaraji radhi za Allah katika amali yake na yale yaliyoko kwake katika malipo na thawabu.

Ni lazima kuhudhurisha nia njema katika kila amali, na katika amali hizo ni wakati wa kuhudumia familia.

التصنيفات

Matumizi.