Mambo manne yatakayekuwa kwake atakuwa mnafiki halisi, na itakayekuwa kwake sifa moja kati ya hizo, atakuwa na sifa ya unafiki mpaka aiache: Akizungumza husema uongo, na akiingia makubaliano hufanya hiyana, na akiahidi anakwenda kinyume, na akigombana huvuka mipaka

Mambo manne yatakayekuwa kwake atakuwa mnafiki halisi, na itakayekuwa kwake sifa moja kati ya hizo, atakuwa na sifa ya unafiki mpaka aiache: Akizungumza husema uongo, na akiingia makubaliano hufanya hiyana, na akiahidi anakwenda kinyume, na akigombana huvuka mipaka

Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Amry -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mambo manne yatakayekuwa kwake atakuwa mnafiki halisi, na itakayekuwa kwake sifa moja kati ya hizo, atakuwa na sifa ya unafiki mpaka aiache: Akizungumza husema uongo, na akiingia makubaliano hufanya hiyana, na akiahidi anakwenda kinyume, na akigombana huvuka mipaka".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Tabia nne amezitahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zitakapokusanyika kwa muislamu atakuwa na mfanano mkubwa na wanafiki kwa sababu ya tabia hizi, na hili linakuwa kwa yule ambaye sifa hizi ndio tabia yake mara kwa mara, ama atakayezifanya mara chache huyu haingii katika sifa hizi, nazo ni: Ya kwanza: Akizungumza husema uongo kwa makusudi na kutokuwa mkweli katika maneno yake. Ya pili: Akitoa ahadi katika makubaliano haitimizi, na humfanyia hiyana aliyeahidiana naye. Ya tatu: Akiahidi ahadi yoyote haitimizi na huenda kinyume. Ya nne: Akizozana na akagombana na yeyote ugomvi wake huwa mkali sana, na hupotoka katika haki, na hufanya hila ya kuipinga na kuibatilisha, na husema maneno ya batili na uongo. Unafiki ni mtu kudhihirisha tofauti na yale anayoyaficha, na maana hii ipo kwa mtu mwenye sifa hizi, na unafiki wake unamuhusu yule anayezungumza naye, na akamuahidi, na akamwamini, na akagombana naye, na akamuahidi mtu, si kwamba atakuwa mnafiki katika Uislamu anaudhihirisha na kuficha ukafiri, hapana, na atakayekuwa na sifa moja katika sifa hizi; basi atakuwa na sifa ya unafiki ndani yake hadi atakapoiacha.

فوائد الحديث

Kumebainishwa baadhi ya alama za mnafiki na tahadhari ya kutoangukia katika unafiki.

Makusudio ya hadithi: Ni kuwa sifa hizi ni sifa za unafiki, na mwenye sifa hizi anafanana na wanafiki kwa sifa hizi, na amejipamba kwa tabia zao, haina maana kuwa ni mnafiki anayedhihirisha Uislamu na kuficha ukafiri, na wamesema baadhi ya wanachuoni kuwa hii inachukuliwa kwa mtu ambaye zitakuwa nyingi kwake sifa hizi na akazipuuzia, na akaziona ndogo; basi atakayekuwa hivyo mara nyingi huwa kaharibika katika itikadi yake.

Amesema Imam Ghazal: Msingi wa dini zote umekusanywa na mambo matatu: Kauli, kitendo, na nia, akatanabahisha kuwa kuharibika kwa maneno ni kwa uongo, na kuharibika kwa vitendo kunakuwa kwa hiyana, na kuharika kwa nia ni kwa kwenda kinyume; kwa sababu kwenda kinyume na ahadi hakumchafui mtu isipokuwa maazimio yake yatakapoambatanishwa na ahadi, ama atakapokusudia kisha kikamtokea kizuizi au akabadili mtazamo huyu hatokuwa na sura ya unafiki.

Unafiki una aina mbili: Unafiki wa kiitikadi unamtoa mtu katika imani, nao ni kudhihirisha Uislamu na kuficha ukafiri, na unafiki wa vitendo, nao ni kujifananisha na wanafiki katika tabia zao, na huu haumtoi mtu katika imani, isipokuwa ni dhambi katika madhambi makubwa.

Amesema bin Hajari: Na wamekubaliana wanachuoni kuwa atakayesadikisha kwa moyo wake na ulimi wake na akafanya mambo haya hahukumiwi kwa ukafiri, wala si mnafiki atakayekaa motoni milele.

Amesema Imam Nawawi: Na wamesema wanachuoni wengi kuwa: Makusudio yake ni wanafiki waliokuwa katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake walizungumza kwa imani yao, na wakapinga, na wakaaminiwa kwa dini yao wao wakafanya hiyana, na wakaahidi katika swala la dini na kuinusuru, wakaenda kinyume, na wakavuka mipaka katika ugomvi wao.

التصنيفات

Unafiki., Kuyasema vibaya Maasi., Matamshi yaliyokatazwa na makosa ya ulimi.