إعدادات العرض
1- Swala nzito juu ya wanafiki: ni swala ya ishaa na swala ya Alfajiri, na lau wangejua yaliyomo ndani ya swala hizo, basi wangeziendea hata kwa kutambaa, na nilitamani niamrishe swala ikimiwe, kisha nimuamrishe mtu awaswalishe watu, kisha niondoke wakiwa pamoja nami wanaume wakiwa na vijinga vya moto twende kwa watu ambao hawahudhurii swala nikazichome nyumba zao kwa moto.
2- Mfano wa mtu mnafiki, ni kama Mbuzi mwenye kutangatanga baina ya makundi mawili ya Mbuzi, wakati mwingine huwa na kundi hili na wakati mwingine huwa na kundi lile