إعدادات العرض
Mfano wa mtu mnafiki, ni kama Mbuzi mwenye kutangatanga baina ya makundi mawili ya Mbuzi, wakati mwingine huwa na kundi hili na wakati mwingine huwa na kundi lile
Mfano wa mtu mnafiki, ni kama Mbuzi mwenye kutangatanga baina ya makundi mawili ya Mbuzi, wakati mwingine huwa na kundi hili na wakati mwingine huwa na kundi lile
Imepokelewa kutoka kwa Bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Mfano wa mtu mnafiki, ni kama Mbuzi mwenye kutangatanga baina ya makundi mawili ya Mbuzi, wakati mwingine huwa na kundi hili na wakati mwingine huwa na kundi lile."
[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]
الترجمة
العربية English မြန်မာ Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands اردو Español Bahasa Indonesia ئۇيغۇرچە বাংলা Türkçe Bosanski සිංහල हिन्दी Tiếng Việt Hausa മലയാളം తెలుగు ไทย پښتو অসমীয়া Shqip دری Ελληνικά Български Fulfulde Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių Malagasy or Română Kinyarwanda Српски тоҷикӣ O‘zbek नेपाली Moore Kurdî Oromoo Wolof Soomaali Français Tagalog Azərbaycan Українська bm தமிழ் Deutsch ქართული Português Македонски Magyar Русский فارسی 中文الشرح
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hali za wanafiki, na kuwa mnafiki ni kama Mbuzi mwenye kutangatanga na asiyejua afuate kundi gani la Mbuzi, wakati mwingine huenda kundi hili na wakati mwingine huenda na kundi lingine, Wanafiki hutangatanga baina ya imani na ukafiri, hivyo hawapo na waumini kwa wazi wazi wala kwa kujificha, wala hawapo na makafiri kwa wazi wala kwa kujificha, bali kwa muonekano wa nje wanaonekana wapo na waumini, na kwa ndani (kwa siri) wapo kwenye shaka na kutanga tanga, wakati mwingine, na wakati mwingine wanaelemea kwa hawa na wakati mwingine kwenye kundi hili.فوائد الحديث
Miongoni mwa miongozo ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kupiga mfano ili kufahamu haraka.
Kuweka wazi hali za wanafiki za kutangatanga kuwa na mashaka na kutokuwa na utulivu.
Kuchukua tahadhari kutokana na hali za wanafiki na kuhimizwa kuwa na imani nje na ndani.
التصنيفات
Unafiki.