Maji yatakapokuwa ni kulataini (Mapipa mawili) basi hayashiki uchafu

Maji yatakapokuwa ni kulataini (Mapipa mawili) basi hayashiki uchafu

Kutoka kwa Abdallah bin Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao amesema: Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu maji, na vile vinavyoyaendea kama wanyama wa kawaida na wanyama pori, akasema rehema na amani ziwe juu yake: "Maji yatakapokuwa ni kulataini (Mapipa mawili) basi hayashiki uchafu".

[Sahihi] [Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na An-Nasaaiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na Ahmad - Imepokelewa na Addaaramy]

الشرح

Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu hukumu ya utwahara wa maji ambayo yanazungukiwa na wanyama wafugwao na wanyamapori kwa ajili ya kunywa na mfano wake, akasema rehema na amani ziwe juu yake kuwa: Maji yakifikia kipimo cha pipa mbili kubwa, ambazo zitakuwa na ujazo wa lita (210) basi hayo ni maji mengi hayawezi kunajisika; isipokuwa ikibadilika kwa najisi moja kati ya sifa zake tatu, rangi yake, au ladha yake au harufu.

فوائد الحديث

Maji yananajisika ikibadilika kwa najisi moja kati ya sifa zake tatu, rangi yake, au ladha yake, au harufu yake, na hadithi imeeleza kwa ujumla na si kwa kuweka kikomo.

Wamekubaliana wanachuoni kuwa maji yakibadilishwa na najisi basi yananajisika moja kwa moja, sawa sawa yawe kidogo au mengi.

التصنيفات

Hukumu za Maji.