إعدادات العرض
Hakika swala hizi mbili, ni swala nzito sana kwa wanafiki, na lau kama mngejua malipo yaliyomo basi mngezijia, hata kwa kutambaa kwa magoti
Hakika swala hizi mbili, ni swala nzito sana kwa wanafiki, na lau kama mngejua malipo yaliyomo basi mngezijia, hata kwa kutambaa kwa magoti
Kutoka kwa Ubai bin Ka'ab radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alitusalisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala ya asubuhi, akasema: "Hivi fulani yupo", Wakasema: Hapana, akasema: "Na je fulani yupo?", Wakasema: Hapana: Akasema: "Hakika swala hizi mbili, ni swala nzito sana kwa wanafiki, na lau kama mngejua malipo yaliyomo basi mngezijia, hata kwa kutambaa kwa magoti, na hakika safu ya kwanza iko katika mithili ya safu ya Malaika, na laiti mngejua ni zipi fadhila zake basi mngezijia haraka mno, na hakika swala ya mtu na mwenzie ni safi zaidi kuliko swala yake peke yake, na swala yake akiwa na watu wawili ni nzuri zaidi kuliko swala yake na mtu mmoja, na wingi unavyozidi ndio unaopendeka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu".
الترجمة
العربية Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Türkçe اردو हिन्दी Tagalog 中文 ئۇيغۇرچە Kurdî Português অসমীয়া አማርኛ ગુજરાતી Tiếng Việt Nederlands සිංහල Hausa پښتو नेपाली ไทย മലയാളം Кыргызча Malagasy Română Svenskaالشرح
Siku moja alisali Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala ya Alfajiri, kisha akauliza: Je, fulani kahudhuria nasi swala yetu hii? Maswahaba wakasema: Hapana. Kisha akasema: Hivi fulani kahudhuria? kwa mtu mwingine, wakasema: Hapana. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika swala ya Alfajiri na Ishaa ni swala nzito kwa wanafiki; kwa sababu ya kuzidi kwa uvivu katika nyakati hizi, na ni kwa sababu ya uchache wa kutoonekana kwa watu, kwa sababu gizani hawaonekani. Na lau kama mngejua enyi waumini yaliyomo ndani ya swala hizi mbili Alfajiri na Ishaa katika malipo na thawabu za ziada, kwa sababu malipo huwa kwa kadiri ya tabu, basi mgeziendea hata kwa kutambaa na kwa kutembea kwa mikono na magoti. Na hakika safu ya kwanza katika ukaribu wake na imam ni kama safu za Malaika ukaribu wake na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na lau waumini wangelijua ni zipi fadhila za safu ya kwanza basi wangeshindana kuiwahi, Hakika swala ya mtu na mtu mwingine inamalipo makubwa na ina athari kubwa kuliko swala yake peke yake, na swala yake pamoja na watu wawili ni bora kuliko swala yake na mtu mmoja, Na swala ambayo waswaliji watakuwa wengi hiyo ndio swala bora inayopendeka kwa Mwenyezi Mungu.فوائد الحديث
Sheria ya imam wa msikiti kukagua hali za waumini, na kumuulizia asiyekuwepo.
Kudumu na swala ya jamaa, na hasa hasa swala ya Ishaa na Alfajiri ni katika alama za imani.
Ukubwa wa malipo ya swala mbili, Ishaa na Alfajiri; kwa sababu kuziendea kunahitaji kupambana na nafsi na kuwa na subira katika utiifu, ikawa malipo yake ni makubwa kuliko swala zingine.
Swala ya jamaa inakamilika kwa kuanzia watu wawili na zaidi.
Kumebainishwa fadhila za safu ya kwanza, na himizo la kuiendea haraka.
Fadhila za wingi wa jamaa, kwani kila wingi unavyokithiri pia malipo huwa mengi.
Amali njema hutofautiana ubora kulingana na kuzidiana sheria yake, na hali zake maalum.