Ewe Abbasi, ewe ami yake na Mjume wa Mwenyezi Mungu, muombe Mwenyezi Mungu afya katika Dunia na Akhera

Ewe Abbasi, ewe ami yake na Mjume wa Mwenyezi Mungu, muombe Mwenyezi Mungu afya katika Dunia na Akhera

Kutoka kwa Al-Abbasi bin Abdil Muttwalib radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nifundishe kitu nitakachomuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu. Akasema: "Muombe Allah afya", nikakaa siku kadhaa kisha nikarudi, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nifundishe kitu ambacho nitamuomba Mwenyezi Mungu. Akasema kuniambia: "Ewe Abbasi, ewe ami yake na Mjume wa Mwenyezi Mungu, muombe Mwenyezi Mungu afya katika Dunia na Akhera".

[Ni sahihi kwa sababu ya hadithi nyingine] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Ahmad]

الشرح

Ami yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake Al-Abbas bin Abdul Muttalib Allah amuwie radhi alimuomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amfundishe dua ya kumuomba Mwenyezi Mungu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamfundisha amuombe Mwenyezi Mungu afya njema na salama kutokana na balaa na kasoro za Dini, Dunia na Akhera, akasema: Baada ya siku chache nikarejea kwake rehema na amani ziwe juu yake kwa mara nyingine tena nikimuomba anifundishe dua nimuombe Mwenyezi Mungu, akasema rehema na amani ziwe juu yake akimwambia kwa mapenzi na upole: Ewe Abbas, ewe ami wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, muombe Mwenyezi Mungu afya aondoe madhara yote na alete kheri na manufaa katika Dunia na Akhera.

فوائد الحديث

Kurudiarudia kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake jibu hilo hilo kwa Abbasi alipomuuliza kwa mara ya pili kunaonyesha afya ndio jambo la heri zaidi mja analomuomba Mola wake Mlezi.

Kumebainishwa fadhila za afya nakuwa imekusanya heri zote katika Dunia na Akhera.

Pupa ya Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao ya kutaka kuongeza elimu na heri.

التصنيفات

Dua zilizopokelewa toka kwa mtume.