Ya kwamba mwanamke mmoja alipatikana akiwa kauwawa katika moja ya vita vya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akakemea vikali Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuuwawa wanawake na watoto

Ya kwamba mwanamke mmoja alipatikana akiwa kauwawa katika moja ya vita vya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akakemea vikali Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuuwawa wanawake na watoto

Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-: Ya kwamba mwanamke mmoja alipatikana akiwa kauwawa katika moja ya vita vya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akakemea vikali Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuuwawa wanawake na watoto.

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliona mwanamke akiwa kauwawa katika moja ya vita, akakemea vikali kuuwawa wanawake na watoto ambao hawajafikia balehe.

فوائد الحديث

Mwanamke na mtoto yeyote ambaye hatopigana, na mwenyekuwa mfano wao kama wazee vikongwe, na watawa, hawa hawauawi, madam hawajatoa rai au msaada wowote wa kuwapiga waislamu, ikiwa watafanya hivyo basi nao watauawa.

Katazo la kuwaua wanawake na watoto; kwa sababu hawa huwa hawawapigi vita waislamu, na malengo ya kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni kuvunja nguvu ya wapiganaji pekee, ili ujumbe wa haki uwafikie watu wote.

Huruma ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake mpaka katika mapambano na vita.

التصنيفات

Adabu za Jihadi.