إعدادات العرض
Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yako nimejisalimisha, na kwako nimeamini, na juu yako nimetegemea, na kwako nimejisogeza, na kwa ajili yako napambana. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kwa utukufu wako hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe najikinga kwa kuto nipoteza, wewe…
Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yako nimejisalimisha, na kwako nimeamini, na juu yako nimetegemea, na kwako nimejisogeza, na kwa ajili yako napambana. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kwa utukufu wako hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe najikinga kwa kuto nipoteza, wewe ndiye uliye hai ambaye hafi, na majini na watu wanakufa
Na imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yako nimejisalimisha, na kwako nimeamini, na juu yako nimetegemea, na kwako nimejisogeza, na kwa ajili yako napambana. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kwa utukufu wako hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe najikinga kwa kuto nipoteza, wewe ndiye uliye hai ambaye hafi, na majini na watu wanakufa".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Hausa Kurdî Tiếng Việt অসমীয়া Nederlands አማርኛ සිංහල ไทยالشرح
Ilikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako nimejisalimisha" na nimenyenyekea, "na kwako nimeamini" na nimesadikisha na nimekiri, "Na juu yako nimetegemea" na nimekabidhi na nimetegemea, "na kwako nimetubia" na nimerejea na nimekuja, "na kwako ninapambana" na ninajibizana kwa hoja na maadui zako, "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajilinda kwako" Ninajiegemeza, "kwa utukufu wako" na ngome yako na ushindi wako, "hapana mola wa haki isipokuwa wewe" na wala hakuna muabudiwa wa haki zaidi yako, "unipoteze" kutoka katika uongofu na taufiki ya kupata radhi zako, "Wewe ndiye uliye hai ambaye hafi" na wala hamaliziki, "na majini na watu wote wanakufa".فوائد الحديث
Sheria ya kutanguliza sifa katika kila mahitaji.
Ulazima wa kutegemea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake na kuomba hifadhi kutoka kwake; kwa sababu yeye ndiye mwenye kusifika kwa sifa kamilifu, basi yeye peke yake yake ndiye mwenye kutegemewa, na viumbe wote hawajiwezi na mwisho wao ni kifo, hivyo wao hawastahiki kutegemewa.
Kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika dua kwa maneno haya yaliyokusanya kila kitu, na yenye kuzuia kingenecho kuingia humo, yanayoelezea kwa imani ya kweli na yakini ya kiwango cha juu.
Amesema As-Sa'diy: Kauli yake: "Wewe ndiye uliye hai" Yaani: Wewe pekee ndiye unayestahiki kuombwa kinga na si mwingine zaidi yako.