Ataletwa mtu siku ya Kiyama, kisha atupwe motoni, ujiviringishe utumbo na vyote vilivyomo tumboni mwake, atazunguka nao (motoni) kama punda anavyozunguka na jiwe la kusagia nafaka

Ataletwa mtu siku ya Kiyama, kisha atupwe motoni, ujiviringishe utumbo na vyote vilivyomo tumboni mwake, atazunguka nao (motoni) kama punda anavyozunguka na jiwe la kusagia nafaka

Kutoka kwa Osama bin Zaidi radhi za Allah ziwe juu yake: Aliambiwa: Je, huingii kwa Othman uzungumze naye? Akasema: Hivi mnadhani kuwa mimi siwezi kumsemesha jambo mpaka nanyi msikie? Wallahi nimekwishamsemesha kwa mambo yaliyo kati yangu na yeye, na wala sitaki kufungua jambo ambalo sihitaji kuwa wa mwanzo kulifungua, na wala sitaki kumueleza yeyote awe kiongozi kwangu: Hakika yeye ni kiongozi baada yakuwa nimemsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Ataletwa mtu siku ya Kiyama, kisha atupwe motoni, ujiviringishe utumbo na vyote vilivyomo tumboni mwake, atazunguka nao (motoni) kama punda anavyozunguka na jiwe la kusagia nafaka, watamkusanyikia watu wa motoni, watamuuliza: We fulani umepatwa na nini? Hivi si ni wewe ulikuwa ukituamrisha mema na kutukataza maovu? Atasema: Ndiyo ni mimi, ila nilikuwa nikiamrisha mema wala siyafanyi, na nikikataza maovu ninayafanya".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Aliambiwa Osama bin Zaid Mwenyezi Mungu awawie radhi wote wawili: Hivi huendi kwa Othman bin Affan, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, ukamwambia kuhusu fitina zilizotokea baina ya watu na kutafuta kuzizima. Basi akawaeleza kuwa alizungumza naye kwa siri ili kutafuta maslahi, si kuchochea kwa fitina, na lengo lake lilikuwa kwamba hataki kuwashutumu viongozi hadharani, ikawa ni sababu ya kurefusha mzozo kwa kiongozi, na ni mlango wa fitina na uovu, na siwezi kuwa wa kwanza kuufungua. Kisha Osama Mwenyezi Mungu awawie radhi, akasema kuwa: Anawanasihi viongozi kwa siri na wala hambembelezi yeyote kwa kumsifu, hata akiwa kiongozi, na wala hawabembelezi kwa kuwasifu kwa uongo, na hiyo ni baada ya yeye kuwa alisikia kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ataletwa mtu Siku ya Kiyama na kutupwa Motoni, na utumbo wake utatoka nje ya tumbo lake kutokana na ukali wa adhabu, na atasokota utumbo wake katika hali hii Motoni kama punda anayezunguka jiwe lake la kusagia nafaka, watu wa Motoni watamzunguka kwa duara kisha watamuuliza: Ewe fulani, je si wewe aliyekuwa ukiamrisha mema na kukataza maovu?! Atasema: Mimi nilikuwa nikiamrisha mema na wala siyafanyi, na ninakataza maovu na ninayafanya.

فوائد الحديث

Asili katika kuwanasihi viongozi inatakiwa iwe kwa siri, na mtu asizizungumze kwa watu wote.

Ahadi ya adhabu kali kwa atakayekwenda kinyume matendo yake na kauli zake

Kua na adabu na viongozi na kuwa wapole kwao, na kuwaamrisha mema na kuwakataza maovu.

Ubaya wa kujipendekeza kwa viongozi katika haki na kudhihirisha kinyume na kile kinachoonekana kama kujipendekeza kwa uongo.

التصنيفات

Sifa za pepo na moto.