Huyo mtu kamkojolea shetani masikioni mwake, au alisema: sikioni kwake

Huyo mtu kamkojolea shetani masikioni mwake, au alisema: sikioni kwake

Kutoka kwa bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Alitajwa mbele ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- mtu aliyelala usiku mpaka pakapambazuka, Akasema: "Huyo mtu kamkojolea shetani masikioni mwake, au alisema: sikioni kwake".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Maana ya hadithi: Anasema bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: "Alitajwa mbele ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- mtu aliyelala usiku mpaka pakapambazuka", Yaani aliendelea kulala na wala hakuamka kusali kisimamo cha usiku, mpaka ikamchomozea alfajiri, Na kauli ya pili: Nikuwa yeye hakuamka kwaajili ya swala ya alfajiri mpaka jua likachomoza. Akasema: "Huyo mtu kamkojolea shetani masikioni mwake" na kauli hii iko kama ilivyo na inabaki katika uhalisia wake; kwasababu imethibiti kuwa shetani anakula na anakunywa na anaoa, Hivyo hakuna kinachozuia asikojoe, na huku ni kumdhalilisha kumfedhehesha kuliko pita kiasi, kuwa shetani kamfanya kuwa choo. Na ametaja masikio pekee pamoja nakuwa jicho ndiyo lilistahiki zaidi kwakuwa hulala ikiwa kama ni ishara ya uzito wa usinginzi, kwasababu masikio ndiyo vyanzo vya kuwa macho na ametaja mkojo pekee; kwasababu ndiyo mwepesi kupenya sehemu zilizo wazi na ni mwepesi kupita katika mishipa ukazalisha uvivu katika viungo vyote.

التصنيفات

Wajibu wa Swala na Hukumu ya Mwenye kuiwacha.