إعدادات العرض
Kuwa duniani kama msafiri au mpitanjia
Kuwa duniani kama msafiri au mpitanjia
kutoka kwa Abdullahi bin Amry -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alishika Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- bega langu, na akasema: "Kuwa duniani kama msafiri au mpitanjia", Na alikuwa bin Omari akisema: Ukishinda mchana usisubiri asubuhi, na ukiamka asubuhi usisubiri jioni, na chukua fursa ya kuitumia vizuri afya yako kwa ajili ya maradhi yako, na uhai wako kwa ajili ya kifo chako.
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Hausa Kurdî Português සිංහල Nederlands অসমীয়া Tiếng Việt ગુજરાતી پښتو Oromoo አማርኛ ไทย Română മലയാളം Malagasy नेपाली Deutsch Кыргызча ქართული Moore Magyar తెలుగు Svenska فارسی Македонскиالشرح
Ibn Omari Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, ameeleza kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimshika begani - nacho ni kiungo cha juu cha mkono na bega - akamwambia: Kuwa katika dunia hii kana kwamba wewe ni mgeni aliyekuja katika nchi ambapo hakuwa na makazi yake, na hakuna wakazi wa kumkaribisha wala familia tegemezi, wala mahusiano ambayo ni sababu ya hili, kuwa shupavu zaidi kuliko mgeni huyu ambaye ni mpita njia anayepita njiani kuelekea katika nchi yake. Kwa sababu mgeni anaweza kuishi katika nchi ya kigeni na akawa mkazi ndani yake, tofauti na msafiri anayetaka kwenda nchini kwake, haja yake huwa ni kupumzika ili apate wepesi na sio kukaa, na kuwa na hamu ya kuwasili katika nchi yake kama vile msafiri hahitaji zaidi ya yale yatakayomfikisha mwisho wa safari yake, halikadhalika muumini katika ulimwengu huu hahitaji zaidi ya yale yatakayomfikisha mahali pazuri. Akazifanyia kazi bin Omari nasaha hizi na alikuwa akisema: Ukiamka usisubiri jioni, na ukishinda mpaka jioni usisubiri asubuhi, na ihesabu nafsi yako kuwa katika wafu walioko makaburini, na kwakuwa umri haukosi moja katika ya mawili, afya na maradhi; fanya haraka siku za afya yako kwa kufanya ibada kwa ajili ya maradhi yako; na tumia fursa ya matendo mema katika wakati wa afya kabla maradhi hayajakuzuia, na faidika na uhai wako katika dunia, kusanya ndani yake yale yatakayokunufaisha baada ya kifo chako.فوائد الحديث
Mwalimu kuweka kiganja chake juu ya bega la mwanafunzi wakati wa kujifunza ni kwa ajili ya kujiliwaza, na kutoa angalizo.
Ni vizuri kuanza kwa nasaha na maelekezo kwa mtu ambaye hajaomba hivyo.
Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kupiga mifano hai yanye kutosheleza, kwa kauli yake: "Kuwa katika dunia kana kwamba ni mgeni au mpitanjia"
Tofauti ya watu katika safari yao ya kwenda Akhera; mpitanjia, hii ni daraja ya juu ya kuipa nyongo dunia kuliko daraja la mgeni.
Kumebainishwa ufupi wa mipango, na maandalizi ya kifo.
Hadithi haimaanishi kuacha riziki na kuharamisha ladha za dunia; lakini inamaanisha ni himizo la kuipa nyongo dunia, na kuihama.
Kwenda mbio katika matendo mema kabla hajashindwa mtu kuyafanya, na kifo au maradhi vikamzuia.
Fadhila za Abdallah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake, kiasi kwamba aliathirika kwa mawaidha kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Makazi ya waumini ni Pepo, muumini ni mgeni katika dunia, na ni msafiri kuelekea Akhera, asiufungamanishe moyo wake na kitu chochote katika mji wa ugenini, bali moyo wake umefungamana na nchi ambayo anarejea kwayo, na kukaa kwake katika dunia ni ili akidhi mahitaji yake na maandalizi yake kwa ajili ya kurejea katika nchi yake.
التصنيفات
Kuzitakasa Nafsi.