إعدادات العرض
Maneno yanayopendeka zaidi kwa Allah ni manne: Sub-haanallah, Al-hamdulillaah, na Laa ilaaha illa llaah, na Allahu Akbar, haidhuru ikiwa utaanza na lolote kati ya hao
Maneno yanayopendeka zaidi kwa Allah ni manne: Sub-haanallah, Al-hamdulillaah, na Laa ilaaha illa llaah, na Allahu Akbar, haidhuru ikiwa utaanza na lolote kati ya hao
Imepokewa kutoka kwa Jundubi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Maneno yanayopendeka zaidi kwa Allah ni manne: Sub-haanallah, Al-hamdulillaah, na Laa ilaaha illa llaah, na Allahu Akbar, haidhuru ikiwa utaanza na lolote kati ya hao".
[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt සිංහල Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు မြန်မာ Русский Deutsch 日本語 پښتو অসমীয়া Shqip Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands ئۇيغۇرچە தமிழ் ไทย دری Fulfulde Magyar ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių or Română Kinyarwanda Српски O‘zbek Moore नेपाली Oromoo Wolof Soomaali Български Українська Azərbaycan ქართული тоҷикӣ Македонски bm Malagasyالشرح
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa maneno yanayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni manne. Sub-haanallaah: Na hili linamaanisha kumtakasa Mwenyezi Mungu na kila aina ya mapungufu. Na Al-hamdulillaah: Nako ni kumsifu Allah kwa ukamilifu uliotimia pamoja na kumpenda na kumtukuza. Na Laa ilaaha illa llaah: Yaani: Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allah. Na Allahu Akbaru: Yaani: Ni Mtukufu mno, na ni Mtakatifu mno kuliko kila kitu. Nakuwa fadhila zake na kupata thawabu zake si lazima kuyapangilia wakati wa kuyatamka.فوائد الحديث
Wepesi wa sheria, kiasi kwamba haidhuru kwa neno lipi kati ya hayo utaanza nalo.
التصنيفات
Adh-kaar zote - mbalimbali.