Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kuondokewa neema zako, na kubadilika kwa afya yako, na kufikiwa ghafla na adhabu zako, na kila aina ya hasira zako

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kuondokewa neema zako, na kubadilika kwa afya yako, na kufikiwa ghafla na adhabu zako, na kila aina ya hasira zako

kutoka kwa Abdullahi bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Ilikuwa miongoni mwa dua za Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kusema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kuondokewa neema zako, na kubadilika kwa afya yako, na kufikiwa ghafla na adhabu zako, na kila aina ya hasira zako"

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliomba kinga ya mambo manne: La kwanza: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajilinda kwako kutokana na kuondokewa na neema zako" za dini na dunia, na nibakie madhubuti ndani ya Uislamu, na najiweka mbali kutoangukia katika maasi yanayoondosha neema. La pili: "Na kubadilika ghafla neema zako" Kubadilika kwake na kuwa balaa; ninakuomba afya isiyo na kikomo, na kusalimika dhidi ya mabalaa na magonjwa. La tatu: "Na kufikwa ghafla na adhabu zako" kama vile balaa au maasi, gharika na adhabu vinapokuja ghafla, huwa hakuna muda wa kutubia na kurekebisha mabaya, na hapa hufikwa na adhabu kali na kubwa mno. La nne: "na hasira zako zote" na sababu zenye kupelekea kupata hasira zako; kwani yeyote utakayemchukia basi atakuwa kapata hasara. Na alileta Mtume rehema na amani ziwe juu yake tamko la wingi; ili likusanye mpaka sababu za hasira zake Aliyetakasika na kutukuka miongoni mwa kauli na matendo na itikadi.

فوائد الحديث

Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhitaji kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Kuomba kinga huku kumeambatana na: Taufiki ya kushukuru neema, na hifadhi ya kutotumbukia ndani ya maasi; kwa sababu huondoa neema.

Pupa ya kujiweka mbali na maeneo ya hasira za Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Aliomba kinga Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutokana na kufikwa ghafla na hasira za Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa sababu akiamua kumlipiza mja kwa mabaya anayoyafanya basi yatamfika mabalaa asiyoweza kuyazuia, na hayazuiliwi na viumbe wengine, hata wakikusanyika wote.

Alijikinga Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutokana na kutoweka kwa afya yake Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa sababu endapo Mungu atampendelea kwa kumpa afya yake, basi atakuwa kapata bahati ya kupata kheri zote za dunia na Akhera, ikimuondokea basi atakuwa kapatwa na shari ya dunia na Akhera, kwani afya ndio sababu ya kutengemaa dini na dunia.

التصنيفات

Dua zilizopokelewa toka kwa mtume.