Hakika Mwenyezi Mungu amewafutia umma wangu yale yanayozungumzwa na nafsi zao, madamu hayajafanyiwa kazi au kuzungumzwa

Hakika Mwenyezi Mungu amewafutia umma wangu yale yanayozungumzwa na nafsi zao, madamu hayajafanyiwa kazi au kuzungumzwa

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu amewafutia umma wangu yale yanayozungumzwa na nafsi zao, madamu hayajafanyiwa kazi au kuzungumzwa".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Muislamu haadhibiwi kwa mazungumzo ya shari ya nafsi yake kabla ya kuyafanyia kazi au kuyazungumza, kiasi kwamba Mwenyezi Mungu ameondolea uzito na kusamehe, na hakuuandikia makosa umma wa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake kwa yale yanayopatikana akilini na yakazunguka katika nafsi bila ya kutulizana nafsi katika hiyo; yakitulizana katika moyo wake, mfano kama kiburi na kujiona au unafiki, au akafanya kwa viungo vyake au akasema kwa ulimi wake basi hapa atahesabiwa.

فوائد الحديث

Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na Kutukuka, ameyaacha na kuyasamehe mawazo na fikira zinazojitokeza katika nafsi, mtu huzungumza mwenyewe ndani ya moyo wake na kupita katika mawazo yake.

Mtu atakapofikiria talaka, na ikapita akilini mwake, lakini akawa hajaitamka na wala hajaiandika, basi hiyo haizingatiwi kuwa ni talaka.

Mazungumzo ya nafsi mtu hahesabiwi vyovyote vile yatakavyokuwa makubwa madam hayajakita ndani ya nafsi yake na akayafanyia kazi au kuyazungumza.

Ukubwa wa cheo cha umma wa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake kwa kufanywa maalum kwa kutokuadhibiwa kwa mazungumzo ya nafsi, kinyume na umma zilizokuwa kabla yetu.

التصنيفات

Matamko ya Talaka.