Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitoa tahlil (Laa ilaaha illa llaah) kwa maneno haya mwisho wa kila swala

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitoa tahlil (Laa ilaaha illa llaah) kwa maneno haya mwisho wa kila swala

Kutoka kwa Abuu Zubairi amesema: Alikuwa bin Zubairi akisema mwisho wa kila swala anapotoa salamu: "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul Mulku walahul-hamdu wahuwa a'laa kulli shai-in qadiir, Laa haula walaa quwwata illaa billaah, Laa ilaaha illa llaah, walaa na'budu illaa iyyaahu, Lahun-ni'matu walahul-fadhlu walahuth-thanaaul hasan, Laa ilaaha illa llaahu Mukhliswiina lahud-diina walau karihal kaafiruun" Na akasema: "Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitoa tahlil (Laa ilaaha illa llaah) kwa maneno haya mwisho wa kila swala".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akinyanyua sauti baada ya salamu ya kila swala ya faradhi kwa dhikri hii tukufu, na maana yake: "Laa ilaaha illa llaahu": Yaani: Hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu. "Wah-dahu Laa shariika lahu" Yaani: Hana ushirika katika Uungu wake na Uumbaji wake na Majina yake na Sifa zake. "Lahul Mulku" Yaani: Ana Ufalme usio na mipaka mpana na ulioenea kila kitu, Ufalme wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo. "Walahul-hamdu" Yaani: Yeye ndiye anasifika kwa ukamilifu usio na kikomo, mwenye kusifika kwa ukamilifu na kwa kupendwa na kutukuzwa kwa hali zote, katika furaha na majonzi. "Wahuwa alaa kulli shai-in qadiir": Uwezo wake umekamilika na umetimia kwa namna zote, hakimshindi kitu, na hakuna jambo lolote linalokataa katika mambo yote. "Laa haulaa walaa quwwata illa billaah" Yaani: Hakuna kugeuka kutoka hali moja kwenda nyingine, na kutoka katika kumuasi Mwenyezi Mungu kuja katika kumtii, na hakuna nguvu ila ni kwa Mwenyezi Mungu Yeye ndiye msaidizi na kwake ndiko kwa kutegemewa. "Laa ilaaha illa llaah, walaa na'budu illa iyyaah": (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, na hatumuabudu yeyote ila Yeye) Huu ni msisitizo wa maana ya Uungu na kukemea shirki, nakuwa hakuna anayestahiki kuabuduiwa zaidi yake. "Lahun-ni'matu wal fadhlu: (Ni mmiliki wa neema na fadhila) Yeye ndiye anaumba neema na kuzimiliki, na humfadhilisha amtakaye katika waja wake. "Walahuth thanaaul hasan" (Na ni zake sifa nzuri): Juu ya dhati yake na sifa zake na matendo yake na neema zake, na kwa kila hali. "Laa ilaaha illa llahu, Mukhliswiina lahud-diin: Hapana Mola mwingine isipokuwa Yeye, tunamtakasia Yeye matendo yote: Yaani: Tunampwekesha si kwa kutaka kujionyesha wala kutaka kusikika katika kumtii Mwenyezi Mungu. "Walau karihal kaafiruun", (Hata kama makafiri watachukia) Yaani: Tumethubutu katika kumpwekesha Mwenyezi Mungu na ibada zake hata kama makafiri watachukia.

فوائد الحديث

Sunna ya kudumu na adhkari za baada ya swala za faradhi.

Muislamu hujifaharisha kwa dini yake, na hudhihirisha nembo zake, hata kama makafiri watachukia.

Linapokuja katika hadithi neno: "Mwisho wa swala", Ikiwa kilichotajwa ndani ya hadithi ni dhikri, basi asili yake hapa ni baada ya salamu, na ikiwa ni dua inakuwa kabla ya salamu ndani ya swala.

التصنيفات

Adh-kaar - yasomwayo- wakati wa swala.