Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi nitakuwa nimemtangazia vita, na hatojiweka karibu kwangu mja kwa kitu ninachokipenda katika vile nilivyomfaradhishia juu yake

Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi nitakuwa nimemtangazia vita, na hatojiweka karibu kwangu mja kwa kitu ninachokipenda katika vile nilivyomfaradhishia juu yake

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Hakika Mwenyezi Mungu amesema: Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi nitakuwa nimemtangazia vita, na hatojiweka karibu kwangu mja kwa kitu ninachokipenda katika vile nilivyomfaradhishia juu yake, na akawa bado mja wangu anaendelea kujiweka karibu yangu kwa ibada za sunna (zisizokuwa za lazima) mpaka nitafikia mahala nitampenda, nikishampenda: Nitakuwa sikio lake analosikilizia, na jicho lake analotazamia, na mkono wake anaoshikia, na mguu wake anaotembelea, na hata akiniomba hakika nitampa, na hata akinitaka kinga hakika nitamlinda, na sijawahi kusita katika jambo lolote ninalotaka kulifanya kama kusita kwangu katika (kuitoa) nafsi ya muumini, hapendi kufa na mimi sipendi kumuudhi".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika hadithil Qudsi yakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Atakayemuudhi kipenzi miongoni mwa vipenzi vyangu na akamkasirisha na akambughudhi basi nitakuwa nimemtangazia uadui. Na walii (Kipenzi) ni: Muumini mchamungu, na kwa kadiri imani na uchamungu wa mja unavyokuwa ndivyo nafasi yake ya ukaribu inavyokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Na hajawahi muislamu kujiweka karibu kwa Mola wake kwa jambo alipendalo zaidi kuliko lile alilomfaradhishia na akamuwajibishia juu yake, ikiwemo kufanya mambo yote ya utiifu, na kuacha maharamisho, na kwa kadiri anavyoendelea muislamu kujikurubisha kwa Mola wake kwa yale ya sunna pamoja na faradhi; mpaka atapata mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu akimpenda, atakuwa akimtimizia mambo yake katika viungo hivi vinne: Atampa umakini katika kusikia kwake, hatosikia ila yale yenye kumridhisha Mwenyezi Mungu. Na humpa umakinifu katika macho yake, hatotazama ila yale anayoyapenda Mwenyezi Mungu kuyatazama na anayaridhia. Na anampa umakinifu katika mkono wake, hatofanya kwa mkono wake ila yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu. Na anampa umakinifu katika mguu wake, hatokwenda ila katika yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu, na wala hatoyaendea ila yale yenye kheri ndani yake. Pamoja na haya yote, akimuomba Mwenyezi Mungu chochote basi Mwenyezi Mungu humpa alichoomba, anakuwa ni mtu mwenye kujibiwa maombi, na ikiwa atataka hifadhi kwa Mwenyezi Mungu na akaomba ulinzi kwake kwa kutaka hifadhi, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu humkinga dhidi ya yale anayoyahofu. Kisha akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na sijawahi kusita katika jambo ninalotaka kulifanya kama kusita kwangu katika kuichukua nafsi ya muumini, kwa kumhurumia; kwa sababu yeye anachukia kifo kwa kuwa ndani yake kuna maumivu, na Mwenyezi Mungu hapendi yanayomuudhi muumini.

فوائد الحديث

Hadithi hii ni miongoni mwa yale anayayopokea Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Mola wake Mlezi, na huitwa Hadithil Qudsi au Ilaahiy, nayo ni ile ambayo lafudhi yake na maana yake inatoka kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa haina umaalum kama Qur'ani ambapo Qur'ani imesifika nao tofauti na maneno mengine, ikiwemo kutumika kisomo chake kama ibada, nakuwa msafi kabla ya kusoma, na changamoto, sayansi zilizomo ndani yake, na mengine mengi.

Katazo la kuwaudhi vipenzi wa Mwenyezi Mungu na himizo la kuwapenda, na kukiri ubora wao.

Amri ya kuwafanyia uadui maadui wa Mwenyezi Mungu na uharamu wa kuwapenda.

Atakayedai uwalii (Kupendwa na) Mwenyezi Mungu pasina kufuata sheria yake huyo ni muongo katika madai yake.

Mapenzi ya Mwenyezi Mungu hupatikana kwa kutekeleza wajibu na kuacha maharamisho.

Miongoni mwa sababu za mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa mja na kujibu maombi yake, ni kutekeleza mambo ya sunna baada ya kutekeleza wajibu na kuacha maharamisho.

Ushahidi juu ya utukufu wa mawalii (Vipenzi wa Mwenyezi Mungu) na daraja zao za juu.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake.