Mtu yeyote atakayesema kumwambia ndugu yake: Ewe kafiri, basi utampata mmoja katika ya hao wawili, ikiwa atakuwa kama alivyosema (litathibiti hilo), na kama si hivyo utarejea kwake

Mtu yeyote atakayesema kumwambia ndugu yake: Ewe kafiri, basi utampata mmoja katika ya hao wawili, ikiwa atakuwa kama alivyosema (litathibiti hilo), na kama si hivyo utarejea kwake

Kutoka kwa bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mtu yeyote atakayesema kumwambia ndugu yake: Ewe kafiri, basi utampata mmoja katika ya hao wawili, ikiwa atakuwa kama alivyosema (litathibiti hilo), na kama si hivyo utarejea kwake".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Amemtahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake muislamu kusema kumwambia ndugu yake muislamu: Ewe kafiri, basi atakuwa kastahiki neno kafiri mmoja wao, na ikiwa ni kweli kama alivyosema (utamthibitikia), na kama si kweli ukafiri utarejea kwa msemaji aliyesema kumwambia ndugu yake.

فوائد الحديث

Amekemewa muislamu kusema kumwambia ndugu yake muislamu mambo asiyokuwa nayo, kama sifa ya uovu na ukafiri.

Tahadhari ya kusema maneno haya machafu, na kwamba msemaji wake yuko katika hatari kubwa atakaposema kumwambia ndugu yake, na lazima kuhifadhi ulimi, na muislamu asizungumze ila kwa elimu.

التصنيفات

Uislamu, Adabu ya mazungumzo na kunyamaza.