“Hakuna Muislamu anayetawadha na akautia vizuri udhu wake, kisha akasimama na kuswali rakaa mbili, akielekea kwa moyo wake na uso wake ndani ya rakaa hizo, isipokuwa Pepo itastahiki kwake.”

“Hakuna Muislamu anayetawadha na akautia vizuri udhu wake, kisha akasimama na kuswali rakaa mbili, akielekea kwa moyo wake na uso wake ndani ya rakaa hizo, isipokuwa Pepo itastahiki kwake.”

Kutoka kwa Uqba bin Amir, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, amesema: “Tulikuwa na zamu ya kuchunga ngamia, basi ikafika zamu yangu nikawapeleka jioni, nikamkuta Mtume rehema na amni ziwe juu yake akiwa amesimama akiwahadithia watu, nikamkuta akiwa katika kauli yake: “Hakuna Muislamu anayetawadha na akautia vizuri udhu wake, kisha akasimama na kuswali rakaa mbili, akielekea kwa moyo wake na uso wake ndani ya rakaa hizo, isipokuwa Pepo itastahiki kwake.” Akasema, nikasema: Ni kheri iliyoje hii, mara ghafla nikasikia msemaji mmoja mbele yangu akisema: Ile ya kabla yake ndio ilikuwa bora, basi nikatazama, mara nikamuona ni Omari, akasema: Nimekuona umekuja hivi karibuni, akasema: “Hakuna yeyote kati yenu atakayetawadha vizuri - au akaukamilisha vizuri- kisha akasema: Nashuhudia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kwamba Muhammad ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, isipokuwa atafunguliwa milango minane ya Pepo, aingie mlango wowote autakao".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Alibainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati akiwaeleza watu fadhila mbili kubwa: Ya kwanza: Mwenye kutawadha vizuri, akaupendezesha vizuri udhu, na akaukamilisha, na akaukamilisha katika namna ilivyoelekezwa, na akakipa kila kiungo haki yake katika maji, kisha akasema: Nashuhudia ya kwamba hakuna mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kwamba Muhammad ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake; Isipokuwa atafunguliwa milango minane ya Peponi, aingie mlango autakao. Pili: Mwenye kutawadha udhu huu kamili, kisha akasimama baada ya udhuu huu na kuswali rakaa mbili; Akiwa ameelekea ndani ya swala kwa moyo wake, kwa ikhlaswi na utulivu, na akanyenyekeza uso wake na viungo vyote vya mwili wake kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa Pepo itakuwa ni wajibu kwake.

فوائد الحديث

Ukubwa wa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kumpa malipo makubwa kwa amali ndogo.

Sheria ya kueneza maji ya udhu na kutawadha kwa ukamilifu, na kuswali rakaa mbili kwa unyenyekevu baada yake, na malipo makubwa yanayopatikana kwayo.

Kueneza maji ya udhu, na kuleta dua hii baada yake, ni katika sababu za kuingia peponi.

Sunna ya kusema dhikiri hii kwa mwenye kuoga pia.

Maswahaba walikuwa na shauku ya kufanya mema, kama vile kujifunza na kusambaza elimu, na ushirikiano wao katika kufanya hivyo na katika masuala ya riziki zao.

Dhikri baada ya kutawadha huutakasa moyo na kuusafisha na ushirikina, kama vile udhuu unavyousafisha mwili na kuuondoa uchafu.

التصنيفات

Sunna na Adabu za Kutawadha