Tulikuwa kwa Omari akasema: "Tumekatazwa kujilazimisha

Tulikuwa kwa Omari akasema: "Tumekatazwa kujilazimisha

Imepokewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Tulikuwa kwa Omari akasema: "Tumekatazwa kujilazimisha".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Anaeleza Omari -Radhi za Allaha ziwe juu yake- kwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwakataza kuyafanya mambo yenye uzito bila kuwa na haja nayo, sawa sawa iwe ni kauli au kitendo.

فوائد الحديث

Miongoni mwa kujikalifisha kuliko katazwa: Kuuliza uliza, au mtu kujikalifisha mambo asiyo na elimu nayo, au akalikazia jambo ambalo Mwenyezi Mungu kalipa nafasi pana.

Ni lazima muislamu ailazimishe nafsi yake wepesi na kutojikalifisha katika kauli na vitendo: Katika kula kwake, na kunywa kwake, na maneno yake, na hali zake zote.

Uislamu ni dini ya wepesi.

التصنيفات

Tabia mbovu.