Amekataza kuweka nadhiri, na akasema: "Hakika nadhiri haiji kwa kheri, bali hutolewa kwayo (vilivyo) kwa bahili

Amekataza kuweka nadhiri, na akasema: "Hakika nadhiri haiji kwa kheri, bali hutolewa kwayo (vilivyo) kwa bahili

Kutoka kwa bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Amekataza kuweka nadhiri, na akasema: "Hakika nadhiri haiji kwa kheri, bali hutolewa kwayo (vilivyo) kwa bahili"

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuweka nadhiri, nayo ni mtu kujiwajibishia kitu ambacho sheria haijamlazimisha kukifanya, na akasema kuwa: Nadhiri haiwahishi kitu na wala haikicheleweshi, bali hutolewa vilivyo kwa mtu bahili ambaye hafanyi ila yale ya wajibu pekee, nakuwa nadhiri haileti kitu ambacho hakikukadiriwa.

فوائد الحديث

Nadhiri si sheria, lakini akiweka nadhiri ni lazima kwake kuitekeleza kama haitokuwa ya maasi.

Sababu ya kuikataza nikuwa (haiji kwa heri); kwa sababu hairejeshi chochote katika kadari za Mwenyezi Mungu; na ili asidhanie mtia nadhiri kuwa kutimia kwa ombi lake kulikuwa kwa sababu ya nadhiri, na Mwenyezi Mungu hana haja na hilo.

Amesema Al-Qurtubi: Makatazo haya mahali pake ni mtu kusema, kwa mfano: Ikiwa Mwenyezi Mungu atamponya mgonjwa wangu, basi nitatoa sadaka kadhaa, lengo lililotajwa hapo juu kuwa ni karaha kufanya hivyo ni kwa sababu alipoweka nia ya utoaji wake ni mpaka litimie lengo fulani, ikaonyesha wazi kuwa hakuwa na nia ya kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu kwa yale aliyoyafanya, bali ametumia njia ambayo ndani yake kuna kubadilishana, na kinacholiunga mkono hili nikuwa lau mgonjwa wake asingepona basi asingetoa sadaka kwa sababu alichokitoa kakiambatanisha na kupona kwake, na hii ni hali ya bakhili, kwani hatoi chochote katika pesa yake isipokuwa kwa kutaka badala ya haraka ya kile alichokitoa kwa kawaida.

التصنيفات

Viapo na Nadhiri.