إعدادات العرض
Atakapofika mmoja wenu katika kikao basi na atoe salamu, na akitaka kunyanyuka pia atoe salamu, kwani ya mwanzo haina haki zaidi kuliko ya mwisho
Atakapofika mmoja wenu katika kikao basi na atoe salamu, na akitaka kunyanyuka pia atoe salamu, kwani ya mwanzo haina haki zaidi kuliko ya mwisho
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapofika mmoja wenu katika kikao basi na atoe salamu, na akitaka kunyanyuka pia atoe salamu, kwani ya mwanzo haina haki zaidi kuliko ya mwisho".
[Ni nzuri] [Imepokelewa na An-Nasaaiy]
الشرح
Alimuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekuja mahali walipokaa watu basi awasalimie, na akitaka kunyanyuka basi awaage jamaa zake pia kwa salamu; kwani salamu ya kwanza wakati wa kuja si bora sana kuliko salamu ya mwisho wakati wa kuondoka.فوائد الحديث
Himizo la kusambaza salamu.
Himizo la kuwasalimia jamaa waliokaa wakati wa kukutana nao na wakati wa kuondoka.
Amesema Assanadi: Kauli yake: "Na akitaka kunyanyuka" Yaani: Kutoka katika kikao, "Salamu Ya mwanzo haina haki zaidi" Yaani: Zote mbili ni sunna halisi zinazotakiwa kufanyiwa kazi, hakuna hiyari ya kuiacha ya pili na kuthibitisha ya kwanza.