Hakuna kuambukizana, wala mikosi ya ndege, wala mkosi wa Bundi, wala mkosi wa Kipanga (Jamii ya ndege). Na mkimbie mwenye ukoma kama unavyomkimbia simba

Hakuna kuambukizana, wala mikosi ya ndege, wala mkosi wa Bundi, wala mkosi wa Kipanga (Jamii ya ndege). Na mkimbie mwenye ukoma kama unavyomkimbia simba

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakuna kuambukizana, wala mikosi ya ndege, wala mkosi wa Bundi, wala mkosi wa Kipanga (Jamii ya ndege). Na mkimbie mwenye ukoma kama unavyomkimbia simba."

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alieleza baadhi ya mambo ya zama za kabla ya Uislamu, kuwa kama ni onyo dhidi yao, na kwa kuwabainishia kuwa amri yote iko mikononi mwa Mwenyezi Mungu, na kwamba hakuna kinachotokea isipokuwa kwa amri yake, na kadari zake, nayo ni: La kwanza: Watu wa zama za kabla ya Uislamu waliamini kwamba ugonjwa huwa unaambukiza peke yake. Kwa hiyo, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akakataza kuamini kwamba ugonjwa huwa una asili ya kuambukiza kutoka kwa mgonjwa kwenda mgonjwa mwingine. Mwenyezi Mungu ndiye mwenye mamlaka ya kuundesha ulimwengu; Na Yeye ndiye anayeteremsha maradhi na kuyaondoa, na halitokei hilo ila kwa kutaka kwake na kwa Kadari Yake. La Pili: Watu wa zama za kabla ya Uislamu walikuwa wakitoka kwa ajili ya safari au biashara walikuwa wanawafukuza ndege, wakiruka kwenda kulia wanafurahi, na wakiruka kushoto wanakata tamaa na kurudi (wakiamini kuwa ni mkosi) basi, Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, akakataza hali hii ya kuamini mikosi kwa sababu ya ndege, na akabainisha kuwa ni imani potofu. Tatu: Watu wa zama za kabla ya Uislamu walikuwa wakisema: Ndege bundi akitua juu ya nyumba, kuna msiba utawapata watu wa nyumba hiyo. Kwa hivyo, akakataza rehema na amani ziwe juu yake, kuamini mikosi katika hilo. Nne: Ni haramu kuamini mwezi wa Swafari kuwa ni mikosi, ambao ni mwezi wa pili katika miezi ya mwandamo. Ilisemekana kuwa Swafari ni: Nyoka tumboni anayeambukiza mifugo na watu, wanadai kuwa anaambukiza zaidi ya upele; akakanusha imani hii. Tano: Aliamrisha kujitenga mbali na mwenye ugonjwa wa ukoma kama vile mtu anavyojiweka mbali na simba. Hii ni kujikinga na kutafuta usalama kwa ajili yake na kufanya sababu alizoamrisha Mwenyezi Mungu, na ukoma ni maradhi ambayo viungo vya mtu hulika.

فوائد الحديث

Umuhimu wa kumwamini na kumtegemea Mwenyezi Mungu, na kufanya sababu za kisheria.

Ni wajibu kuamini hukumu na Kadari ya Mwenyezi Mungu, na kwamba sababu ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu na Yeye ndiye anayezifanya zitokee au kuondoa athari zake.

Kubatilika kwa baadhi ya mambo wanayoyafanya baadhi ya watu kwa kupima bao kwa kutumia rangi, kama vile nyeusi na nyekundu, au namba fulani, na majina, na watu wenye ulemavu.

Katika kukataza ukaribu na wenye ukoma na wale walio na magonjwa ya kuambukiza; Ni moja ya sababu ambazo Mwenyezi Mungu aliweka desturi kuwa zinapelekea katika matokeo yake. Sababu hazijitegemei zenyewe binafsi, bali ni Mwenyeezi Mungu ambaye, Akitaka, Anaziondoa nguvu zake, kwa hivyo haziwezi kuathiri chochote, na Akitaka, Anazibakisha, hivyo zitaweza kuathiri.

التصنيفات

(Mambo ya kale kabla ya uislamu), Matendo ya moyoni.