إعدادات العرض
Hakika Mwenyezi Mungu amepanga mema na mabaya, kisha akalibainisha hilo, atakayekusudia kufanya jema akawa hakulifanya Mwenyezi Mungu humuandikia jema moja kamili, ikiwa atapania na akalifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake mema kumi mpaka ziada ya mia saba, mpaka kufikia nyongeza ya juu zaidi, na…
Hakika Mwenyezi Mungu amepanga mema na mabaya, kisha akalibainisha hilo, atakayekusudia kufanya jema akawa hakulifanya Mwenyezi Mungu humuandikia jema moja kamili, ikiwa atapania na akalifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake mema kumi mpaka ziada ya mia saba, mpaka kufikia nyongeza ya juu zaidi, na atakayekusudia jambo baya na akawa hakulifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake jema moja kamili, ikiwa atapania na akalifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake dhambi moja
Imepokewa Kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake- Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika yale anayoyapokea kutoka kwa Mola wake Mtukufu amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu amepanga mema na mabaya, kisha akalibainisha hilo, atakayekusudia kufanya jema akawa hakulifanya Mwenyezi Mungu humuandikia jema moja kamili, ikiwa atapania na akalifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake mema kumi mpaka ziada ya mia saba, mpaka kufikia nyongeza ya juu zaidi, na atakayekusudia jambo baya na akawa hakulifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake jema moja kamili, ikiwa atapania na akalifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake dhambi moja."
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Bahasa Indonesia Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Français Tiếng Việt Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు தமிழ் မြန်မာ Русский Deutsch 日本語 پښتو অসমীয়া Shqip Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands ئۇيغۇرچە සිංහල ไทย دری Fulfulde Magyar Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių or Română Kinyarwanda Српски тоҷикӣ O‘zbek Moore नेपाली Oromoo Wolof Soomaali Български Українська Azərbaycan bm ქართული lnالشرح
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu amepanga mema na maovu, kisha akawabainishia Malaika wawili ni namna gani watayaandika: Atakayetaka na akakusudia na akaazimia kufanya jema basi litaandikwa kwake jema moja, hata kama hatolifanya, na ikiwa atalifanya basi hulipwa mara dufu kwa mara kumi mfano wake, mpaka ziada ya mia saba, mpaka ziada nyingi zaidi, na ziada huendana na yale yaliyoko moyoni kwanzia Ikhlaswi (kutakasa nia) na kuwanufaisha wengine, n.k. Na atakayetaka na akakusudia na akaazimia kufanya uovu kisha akauacha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, huanidikiwa jema moja, na ikiwa atauacha kwa sababu ya kukosa muda wa kuufanya na akiwa hajafanya sababu za kuuendea, hatoandikiwa chochote, na akiuacha kwa kushindwa huandikwa nia yake pekee, na ikiwa ataufanya litaandikwa kwa ovu moja.فوائد الحديث
Kumebainishwa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya Umma huu katika kuzidishiwa mema na kuandikwa kwake, na kutozidishwa maovu.
Umuhimu wa nia katika amali zote na athari yake.
Fadhila za Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- na upole wake na ihisani yake nikuwa mwenye kudhamiria jema na akawa hakulifanya Allah huliandika jema kamili.