إعدادات العرض
Atakayefunga siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, atauweka mbali Mwenyezi Mungu uso wake na moto miaka sabini
Atakayefunga siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, atauweka mbali Mwenyezi Mungu uso wake na moto miaka sabini
Imepokelewa na Abii Said Al-khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayefunga siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, atauweka mbali Mwenyezi Mungu uso wake na moto miaka sabini".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Português Kurdî සිංහල Tiếng Việt অসমীয়া ગુજરાતી Nederlands አማርኛ ไทย മലയാളം Românăالشرح
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayefunga siku moja katika Jihadi na kwingineko kwa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa kutafuta thawabu na malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu; basi Mwenyezi Mungu kwa fadhila zake ataweka mbali baina yake na moto miaka sabini.فوائد الحديث
Amesema Nawawi: Fadhila za kufunga katika njia ya Mwenyezi Mungu, na hili linachukuliwa kwa yule ambaye hadhuriki kwa swaumu hiyo, na wala hapotezi haki zake, na wala hatopoteza mapambano yake wala kinginecho katika majukumu mapigano yake.
Himizo na hamasisho la kufunga swaumu ya hiyari.
Uwajibu wa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na wala asifunge kwa kujionyesha wala kutaka kusikika, wala kwa makusudio mengine.
Amesema As-sanadi: Kauli yake "Katika njia ya Mwenyezi Mungu", inategemea kuwa masukudio yake ni nia pekee, na inawezekana kuwa makusudio yake nikuwa amefunga akiwa katika hali ya vitani, na la pili ndio liko karibu na usawa.
Amesema bin Hajari: Kauli yake: "Viangazi sabini" Kiangazi ni wakati maalumu wa mwaka, na makusudio yake hapa ni mwaka, na kutajwa kiangazi pekee hapa pasina kutaja wakati uliobakia -kama kiangazi na masika, na kipupwe-; kwa sababu kiangazi ndio kipindi kizuri zaidi kwani hua ndio muda wa kuvuna matunda.
التصنيفات
Funga za Kujikurubisha.