Si halali damu ya muislamu isipokuwa kwa moja kati ya mambo matatu

Si halali damu ya muislamu isipokuwa kwa moja kati ya mambo matatu

Kutoka kwa bin Mas'udi radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake-: "Si halali damu ya muislamu isipokuwa kwa moja kati ya mambo matatu: Mzinifu aliyeoa, na nafsi kwa nafsi, na mwenye kuacha dini yake mwenye kusambaratisha umoja".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa damu ya Muislamu ni haramu, isipokuwa akifanya moja katika mambo matatu: La kwanza: Akatakayetumbukia katika uchafu wa zinaa, na hali yakuwa ameoa ndoa sahihi ya kisheria; ni halali kumuua kwa mpiga mawe. La pili: Atakayeua nafsi isiyo na hatia kwa makusudi pasina haki, atauwawa kwa sharti zake. La tatu: Mwenye kutoka katika umoja wa Waislamu; ima kwa kuacha dini yake ya Uislamu yote kwa kuritadi, au mwenye kutoka bila kuritadi kwa kuacha sehemu ya dini kama waasi, na vibaka, na wanaopiga vita Waislamu kama Makhawariji na wengineo.

فوائد الحديث

Uharamu wa kufanya mambo haya matatu, na kuwa atakayefanya moja miongoni mwa hayo atastahiki adhabu ya kifo: Ima kwa sababu ya kukufuru, naye ni yule anayeritadi na kutoka katika Uislamu, na ima kwa kusimamishiwa sheria, nao ni wawili: Mzinifu aliyeoa, na mwenye kuua makusudi.

Ulazima wa kuhifadhi heshima na kuzitakasa.

Uwajibu wa kumuheshimu Muislamu, na kwamba damu yake imelindwa.

Himizo la kushikamana na umoja wa Waislamu na kutofarakana nao.

Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kiasi ambacho huja maneno yake wakati mwingine kwa migawanyiko; kwa sababu migawanyiko hukusanya mambo na kuyaweka pamoja na ni rahisi sana kuyahifadhi.

Mwenyezi Mungu ameweka sheria ya mipaka; ili kumkemea mwenye kufanya, na kwa ajili kuilinda jamii na kuikinga dhidi ya uhalifu.

Kutekeleza sheria hizi ni katika mambo maalumu kwa kiongozi pekee.

Sababu za kuuwa ziko zaidi ya tatu, lakini hazitoki nje ya hizo tatu, amesema Ibinil-Arabi Al-Maaliki: Na hazitoki nje ya sababu hizi tatu kwa namna yoyote ile, kwani atakayeroga au akamtukana Mtume wa Mwenyezi Mungu atakuwa amekufuru, atakuwa ameingia katika yule mwenye kuiacha dini yake.

التصنيفات

Hukumu za (Haddi)_Adhabu zilizopangwa kisheria.