Wasikilizeni na muwatii, kwani wao wana yao waliyobebeshwa nanyi mna yenu mliyobebeshwa

Wasikilizeni na muwatii, kwani wao wana yao waliyobebeshwa nanyi mna yenu mliyobebeshwa

Kutoka kwa Wail bin Hadhrami amesema: Salama bin Yazidi Al-Ju'fi radhi za Allah ziwe juu yake alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu, hebu tueleze endapo watasimama viongozi wetu wakituomba haki zao, na hali wao wanazuia haki zetu, unatuamrisha nini? Mtume akampuuza, kisha akamuuliza, akampuuza, kisha akamuuliza katika mara ya pili au ya tatu, Ash'athi bin Kaisi akamvuta, na akasema: "Wasikilizeni na muwatii, kwani wao wana yao waliyobebeshwa nanyi mna yenu mliyobebeshwa"

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu viongozi wanaotaka haki zao kwa watu ikiwemo kusikilizwa na kutiiwa, na wanazuia haki zilizo juu yao; kama kutenda uadilifu na kuwapa watu ngawira na kurejesha mali za dhulma na kufanya usawa, unatuamrisha tufanye nini tukiwa pamoja nao?. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akampuuza; kana kwamba kalichukia swali hili, lakini muulizaji akarudia mara ya pili na ya tatu, Ash'athi bin Kaisi akamvuta muulizaji ili amnyamazishe. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akajibu na akasema: Sikilizeni kauli zao, na mtii amri zao; kwani wana yao waliyobebeshwa na kulazimishwa kuyafanya ikiwemo uadilifu na raia kuwapa haki zao, na nyinyi mna yenu mliyobebeshwa kama kutii na kutimiza haki na kusubiri juu ya mabalaa.

فوائد الحديث

Amri ya kusikia na kutii kwa viongozi kwa kila hali katika yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, hata wasipotekeleza haki za raia.

Uzembe wa viongozi katika kutimiza wajibu wao, haupelekei watu wengine kufanya uzembe ili kulipiza kisasi katika wajibu wao; kila mmoja ataulizwa juu ya matendo yake, na atahukumiwa kwa uzembe wake.

Dini haijajengwa katika misingi ya nipe nikupe, bali katika misingi ya kushikamana na yale ya wajibu hata kama mtu mwingine hatotenda haki kwa yale ya wajibu kwake kwa wakati huo, kama ilivyokuja katika hadithi hii.

التصنيفات

Haki ya kiongozi kwa Raia.