إعدادات العرض
Hivi mnajua ni nini kusengenya?", Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi, akasema: "Ni kumsema ndugu yako kwa yale anayoyachukia
Hivi mnajua ni nini kusengenya?", Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi, akasema: "Ni kumsema ndugu yako kwa yale anayoyachukia
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hivi mnajua ni nini kusengenya?", Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi, akasema: "Ni kumsema ndugu yako kwa yale anayoyachukia", Pakasemwa: Waonaje ikiwa niyasemayo yako kwa ndugu yangu? Akasema: "Yakiwa kwake uyasemayo utakuwa umemsengenya, na ikiwa hana basi utakuwa umemzulia uongo".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు தமிழ் မြန်မာ Deutsch 日本語 پښتو Tiếng Việt অসমীয়া Shqip Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands ئۇيغۇرچە සිංහල ไทย دری Fulfulde Magyar Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių or Română Kinyarwanda Српски O‘zbek Moore नेपाली тоҷикӣ Oromoo Wolof Soomaali Malagasy Български Українська Azərbaycan ქართული bm Lingala Македонскиالشرح
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ukweli kuhusu kusengenya kuliko haramishwa, nako ni: Kumsema muislamu asiyekuwepo kwa yale anayoyachukia, sawa sawa iwe ni katika sifa zake za kimaumbile au za kitabia, mfano: Chongo, mpiga ghushi, muongo, na mfano wa hayo katika sifa mbaya, hata kama sifa hizo anazo. Ama zisipokuwa kwake sifa hizo hii ndio mbaya zaidi kuliko kusengenya, nako ni kuzua uongo, yaani: kumzulia mtu asiyokuwa nayo.فوائد الحديث
Uzuri wa mafundisho ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kiasi kwamba hutoa mafundisho kwa njia ya swali.
Uzuri wa adabu ya Masahaba wakiwa pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, waliposema: Mwenyezi Mungu na Mtume ndio wajuzi.
Kauli ya muulizwaji kwa lile asilolijua: Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi.
Sheria imelinda jamii, na imehifadhi haki na udugu baina yao.
Kusengenya ni haramu isipokuwa katika baadhi ya hali kwa ajili ya masilahi; Na miongoni mwake: Ni kuzuia dhulma, kiasi kwamba atamtaja aliyedhulumiwa yule aliyemdhulumu kwa yule anayeweza kumchukulia haki yake, akasema: Fulani kanidhulumu, au kanifanyia jambo hili na lile, ikiwemo pia kutaka ushauri katika swala la kuoa au ushirika au ukaribu, na mfamo wake.
التصنيفات
Adabu ya mazungumzo na kunyamaza.