Atakayekwenda asubuhi msikitini au mchana, Mwenyezi Mungu humuandalia nyumba peponi kila anapotoka asubuhi au jioni

Atakayekwenda asubuhi msikitini au mchana, Mwenyezi Mungu humuandalia nyumba peponi kila anapotoka asubuhi au jioni

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayekwenda asubuhi msikitini au mchana, Mwenyezi Mungu humuandalia nyumba peponi kila anapotoka asubuhi au jioni"

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Amempa habari njema Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kwenda msikitini kwa ajili ya ibada au elimu kwa lengo jingine katika mambo ya kheri katika wakati wowote; mwanzo wa mchana au mwisho wake kuwa Mwenyezi Mungu amemuandalia mahali na takrima ya ugeni peponi, kila anapokuja msikitini usiku au mchana.

فوائد الحديث

Fadhila za kwenda msikitini, na himizo la kuhifadhi swala ya jamaa ndani ya msikiti, kwani anapitwa na daraja ngapi mwenye kukwepa kwenda msikitini na kheri na fadhila na malipo na ugeni aliouandaa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa mwenye kwenda katika nyumba yake.

Ikiwa watu humkirimu anayewajia katika majumba yao, na kumletea chakula, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mkarimu zaidi kuliko viumbe wake! Yeyote atakayekwenda katika nyumba yake basi atamkirimu, na Mwenyezi Mungu atamuandalia mafikio ya thamani na yenye nafasi kubwa.

Furaha na moyo mkunjufu wakati wa kwenda msikitini; kwa sababu anaandaliwa makazi kila anapokwenda asubuhi au mchana kwa idadi ya kwenda kwake.

التصنيفات

Ubora wa Swala ya Jamaa na Hukumu zake.