Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe mimi makosa yangu, na ujinga wangu, na ubadhirifu wangu katika jambo langu lote, na yale unayoyajua kutoka kwangu, ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu, na yale ya makusudi na ujinga wangu na mzaha wangu, na hayo yote yaliyo kwangu, ewe Mola wangu nisamehe…

Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe mimi makosa yangu, na ujinga wangu, na ubadhirifu wangu katika jambo langu lote, na yale unayoyajua kutoka kwangu, ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu, na yale ya makusudi na ujinga wangu na mzaha wangu, na hayo yote yaliyo kwangu, ewe Mola wangu nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza, wewe ndiye muwahishaji na wewe ndiye mcheleweshaji, na wewe juu ya kila kitu ni muweza

Kutoka kwa Abuu Mussa radhi za Allah ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakwamba yeye alikuwa akiomba kwa dua hii: "Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe mimi makosa yangu, na ujinga wangu, na ubadhirifu wangu katika jambo langu lote, na yale unayoyajua kutoka kwangu, ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu, na yale ya makusudi na ujinga wangu na mzaha wangu, na hayo yote yaliyo kwangu, ewe Mola wangu nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza, wewe ndiye muwahishaji na wewe ndiye mcheleweshaji, na wewe juu ya kila kitu ni muweza".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ilikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake zilizokusanya mambo mengi ni kauli yake: "Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe makosa yangu" "na dhambi zangu", na yale yaliyotokea kwangu pasina kujua. "Na ubadhirifu wangu katika jambo langu lote" na uzembe wangu na kuvuka kwangu mipaka. "Na yale uyajuayo kutoka kwangu" Uliyoyajua ewe Mwenyezi Mungu lakini mimi nimeyasahau. "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe makosa yangu na makusudi yangu" Na yale yaliyotokea kwa makusudi na kwa kujua kwangu kuwa ni dhambi. "Na niliyodhamiria na yale ya mzaha" Na yale yaliyotekea kwa mzaha, na yale yaliyotokea katika hali zote mbili. "Na hayo yote toka kwangu" Kiasi kwamba yote yaliyotajwa yamekusanya madhambi na aibu zote. "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe niliyoyatanguliza" Katika yale yaliyopita, "Na yale niliyoyachelewesha" Katika yale yatakayokuja. "Na yale niliyoyafanya kwa siri" niliyoyaficha "Na niliyoyatangaza" Na kuyaonyesha wazi. "Wewe ndiye muwahishaji na wewe ndiye mcheleweshaji" Unamtanguliza umtakaye katika viumbe wako katika rehema zako kwa kumpa taufiki katika yale unayoyaridhia, na wewe ndiye unayemchelewesha umtakaye katika hilo, kwa kumnyima uwezo, hakuna wa kuyapeleka mbele uliyoyachelewesha, na wala hakuna kuyachelewesha mambo uliyoyawahisha. "Na wewe juu ya kila kitu ni muweza" Yaani: Unauwezo uliokamilika na maamuzi timamu, mfanyaji pasina kizuizi cha yote uyatakayo.

فوائد الحديث

Fadhila za dua hii, na kuipupia kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Katazo la kufanya ubadhirifu nakuwa mbadhirifu amejiingiza katika adhabu.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anamjua mwanadam vizuri zaidi kuliko anavyojijua, hivyo anatakiwa akabidhi mambo yake kwa Mwenyezi Mungu; kwani yeye anaweza kukosea pasina kujua.

Mwanadam anaweza kuchukuliwa hatua kwa sababu ya mzaha wake kama anavyochukuliwa katika kukusudia kwake, hivyo ni wajibu kwa mwanadam achukue tahadhari katika mzaha wake.

Amesema bin Hajari Al-Asqalaani: Sijaona chochote katika njia za mapokezi ya hadithi hii kuwa dua hii inasomwa mahala fulani, na riwaya zimekuja nyingi zikionyesha mwisho wake... kama kusema ndani ya swala za usiku, na riwaya za mapokezi zimetofautiana, je alikuwa akiisoma kabla ya salaam au baada yake? Na zote mbili zimeelezwa.

Je, Mtume rehema na amani ziwe juu yake anakosea na kuomba msamaha? Imesemekana kuwa alisema hivyo kwa unyenyekevu na kwa kuitenza nguvu nafsi yake, na akachukulia kuwa kupitwa na ukamilifu na kuacha kilicho bora ni dhambi, au alikusudia yale yanayotokea kwa kusahau, au yale yaliyotokea kabla ya utume, na imesemwa kuwa: Kutaka msamaha ni ibada hivyo ni lazima kuileta, si kwa sababu ya kutaka kusamehewa pekee, bali ni kwa kumuabu Mwenyezi Mungu, na imesemwa kuwa: Hili ni angalizo na ni funzo kwa umma wake; ili wasijiaminishe na wakaacha kuomba msamaha.

التصنيفات

Dua zilizopokelewa toka kwa mtume.