Hakuna kitu kinachotukuzwa zaidi kwa Allah Mtukufu kuliko dua

Hakuna kitu kinachotukuzwa zaidi kwa Allah Mtukufu kuliko dua

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna kitu kinachotukuzwa zaidi kwa Allah Mtukufu kuliko dua".

[Ni nzuri] [Imepokelewa na Ibnu Maajah]

الشرح

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna chochote katika ibada kilicho bora zaidi mbele ya Allah Mtukufu kuliko dua; kwa sababu ndani yake kuna kukiri utajiri wa Allah Mtukufu, na kukiri kushindwa kwa mja na kuhitajia kwake kutoka kwake.

فوائد الحديث

Ubora wa dua nakuwa mwenye kumuomba Allah basi huwa kamtukuza, na amekiri kuwa Yeye ni mkwasi -Aliyetakasika- kwani Masikini haombwi, nakuwa Yeye ni Msikivu, kwani kiziwi haombwi, nakuwa Yeye ni mkarimu, kwani bahili haombwi, nakuwa yeye anahuruma, kwani mkorofi haombwi, nakuwa Yeye anaweza, kwani asiyejiweza haombwi, nakuwa Yeye yuko karibu, kwani aliyembali hasikii, na zinginezo katika sifa za utukufu na za uzuri wa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na Kutukuka-.

التصنيفات

Fadhila za Dua., Fadhila za Dua.