Ogopeni dhulma, kwa hakika dhulma ni giza siku ya kiyama. Na ogopeni tamaa, kwa hakika tamaa iliwaangamiza walio kuwepo kabla yenu

Ogopeni dhulma, kwa hakika dhulma ni giza siku ya kiyama. Na ogopeni tamaa, kwa hakika tamaa iliwaangamiza walio kuwepo kabla yenu

Na kutoka kwa Jaabir Bin Abdillah -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- "Ogopeni dhulma, kwa hakika dhulma ni giza siku ya kiyama. Na ogopeni tamaa, kwa hakika tamaa iliwaangamiza walio kuwepo kabla yenu. Iliwapelekea kumwaga damu zao, na kuhalalisha yaliyo haramu kwao".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Alitahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu dhulma, ikiwemo: Kuwadhulumu watu na kujidhulumu mwenyewe na kufanya dhulma katika haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, nayo kuacha kumpa kila mwenye haki haki yake, nakuwa dhulma ni giza kwa wafanyaji dhulma siku ya Kiyama ikiwemo kupata matatizo na misukosuko, Na akakataza tamaa ambayo ni ubahili uliopitiliza pamoja na pupa, na ikiwemo kufanya uzembe katika kutekeleza haki ya mali na tamaa iliyopitiliza ya kuipupia dunia, Na aina hii ya dhulma iliwaangamiza Umma waliokuwa kabla yetu, kiasi ambacho iliwapelekea kuuana wao kwa wao, na kuyahalalisha yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu katika mambo yaliyoharamishwa.

فوائد الحديث

Kutoa mali na kuwaliwaza ndugu ni katika sababu za kupendana na kuwa na mawasiliano.

Ubahili na tamaa huwavuta watu katika maasi na machafu na madhambi.

Kuchukua mazingatio kupitia hali za wale waliotangulia.

التصنيفات

Mambo mazuri na Adabu- Heshima., Tabia mbovu.