Liepukeni chafu hili alilolikataza Mwenyezi Mungu, atakayetumbukia katika hilo basi ajifiche kwa stara ya Mwenyezi Mungu na atubie kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu atakayetufungulia ukurasa wake tutamsimamishia kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu

Liepukeni chafu hili alilolikataza Mwenyezi Mungu, atakayetumbukia katika hilo basi ajifiche kwa stara ya Mwenyezi Mungu na atubie kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu atakayetufungulia ukurasa wake tutamsimamishia kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu

Kutoka kwa Abdallah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisimama baada ya kumuadhibu kwa kumpiga mawe Al-Aslami, akasema: "Liepukeni chafu hili alilolikataza Mwenyezi Mungu, atakayetumbukia katika hilo basi ajifiche kwa stara ya Mwenyezi Mungu na atubie kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu atakayetufungulia ukurasa wake tutamsimamishia kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu".

[Sahihi] [Imepokelewa na Albayhaqy - Imepokelewa na Al Haakim]

الشرح

Ameeleza Omari radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisimama baada ya kumpopoa mawe Maaizi bin Malik Al-Aslami radhi za Allah ziwe juu yake, kwa adhabu ya zinaa, akawahutubia watu, na akasema: Jiepusheni na chafu hili na yote yanayotia kinyaa na machafu miongoni mwa maasi aliyoyakataza Mwenyezi Mungu, na atakayeangukia na akafanya chochote basi ni wajibu kwake mambo mawili: La kwanza: Ajifiche katika mahali alipomsitiri Mwenyezi Mungu, na asimueleze yeyote kuhusu maasi yake. La pili: Afanye haraka kutubia kwa Mwenyezi Mungu na wala asiendelee, na yatakayeonekana wazi maasi yake basi tutamsimamishia sheria iliyotajwa ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mwenyezi kwa maasi hayo.

فوائد الحديث

Himizo la mja mkosefu kujisitiri, na atubie dhambi kwa yale yaliyo baina yake na Mola wake Mlezi.

Mipaka ya Mwenyezi Mungu inapomfikia kiongozi mkuu ni lazima atekeleze adhabu hiyo.

Ulazima wa kuyaepuka maasi, na kutubia dhidi yake.

التصنيفات

Toba