Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hajui kitenganishi kati ya Sura na Sura nyingine mpaka imteremkie {Bismillahir Rahmanir Rahiim}

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hajui kitenganishi kati ya Sura na Sura nyingine mpaka imteremkie {Bismillahir Rahmanir Rahiim}

Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hajui kitenganishi kati ya Sura na Sura nyingine mpaka imteremkie {Bismillahir Rahmanir Rahiim}.

[Sahihi] [Imepokelewa na Abuu Daud]

الشرح

Anaweka wazi Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: kuwa Sura za Qur'ani tukufu zilikuwa zikiteremka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- haikuwa ikijulikana kitenganishi chake wala mwisho wake mpaka imteremkie: {Bismillahir Rahmanir Rahiim} basi wakati huo ndipo hujua kuwa Sura iliyotangulia imekwisha, na hiyo Bismillahi ni mwanzo wa Sura mpya.

فوائد الحديث

Bismillah hutumika kuzitenganisha Sura, isipokuwa kati ya Suratul Anfaal na Suratu t-taubah.

التصنيفات

Kuteremka Qur'an na kukusanywa kwake., Ukusanyaji wa Qur'an.