Hakuna mwenye kumiliki dhahabu wala fedha, na akawa hazitolei zaka zake, isipokuwa, pindi itakapofika siku ya Kiyama, atakunjiwa Sahani la kutoka motoni

Hakuna mwenye kumiliki dhahabu wala fedha, na akawa hazitolei zaka zake, isipokuwa, pindi itakapofika siku ya Kiyama, atakunjiwa Sahani la kutoka motoni

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakuna mwenye kumiliki dhahabu wala fedha, na akawa hazitolei zaka zake, isipokuwa, pindi itakapofika siku ya Kiyama, atakunjiwa Sahani la kutoka motoni, basi litachemshwa katika moto wa Jahanam, kisha zitapigwa pasi mbavu zake na paji lake la uso na mgongo wake, kila linapopoa linarejeshewa umoto, katika siku ambayo makadirio yake yatakuwa ni miaka elfu hamsini, (atadumu katika adhabu hiyo) mpaka watu watakapohukumiwa, naye akaona njia yake, ima inakwenda peponi, na ima anakwenda motoni"

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amebainisha makundi ya mali, na malipo ya mtu ambaye hatotekeleza zaka yake siku ya Kiyama, na miongoni mwake: Ya kwanza: Dhahabu na fedha na vyote vilivyo katika hukumu ya hivyo miongoni mwa mali na bidhaa za biashara, nazo ni zile za wajibu ndani yake kutolewa zaka ikawa hazikutekelezwa, itakapofika siku ya Kiyama zitayeyushwa na kumiminwa na kutengenezwa katika umbile la sahani, na zitawashwa na kuchemshwa katika moto wa Jahannam, na ataadhibiwa nazo mwenye nazo, zitapigwa pasi kwazo mbavu zake na paji lake la uso na mgongo wake, kila ikipoa inachemshwa tena, na ataendelea katika hali hii ya adhabu kwa muda wote wa siku ya Kiyama ambao makadirio ya siku yake ni siku elfu hamsini, mpaka Mwenyezi Mungu atakapohumu kati ya viumbe, hapo ima awe ni katika watu wa peponi au watu wa motoni. Wa pili: Ni mmiliki wa ngamia ambaye hatekelezi faradhi ya zaka zake na haki zake, ikiwemo kuwakamua na kumpatia maziwa anayehudhuria wakati wa kukamua miongoni mwa masikini, wataletwa ngamia hawa wakiwa wakubwa tena walionenepa, na wakiwa wengi kwa idadi zaidi ya jinsi walivyokuwa, na mmiliki wake atatupwa na kulazwa chini na kunyooshwa vizuri siku ya Kiyama katika Ardhi pana ya tambarare, watakuwa wakimkanyaga kwa miguu yao na wakimng'ata kwa meno yao, kila akipita wa mwisho wao, anarejeshwa wa mwanzo wao, na ataendelea katika hali hii ya adhabu kwa muda wote wa siku ya Kiyama ambayo kiasi chake ni siku elfu hamsini, mpaka Mwenyezi Mungu atakapohukumu baina ya viumbe, na hapo atakuwa ni miongoni mwa watu wa peponi au watu wa motoni. Wa tatu: Ni mmiliki wa ng'ombe na mbuzi -ikiwemo kondoo- ambazo mmiliki wake hatekelezi zaka yake ya faradhi, zitaletwa zikiwa kamili kwa wingi zaidi ya jinsi zilivyokuwa, hakuna mnyama atakayepungua, atanyooshwa vizuri na kutupwa na atalazwa huyo mmiliki wake siku ya Kiyama katika Ardhi pana ya tambarare, hakuna mnyama atakayekuwa na pembe zilizopinda, wala asiyekuwa na pembe, wala aliyevunjika pembe, bali watakuwa katika maumbile yao kamili, watakuwa wakimchoma kwa pembe zao, na wakimkanyaga kwa miguu yao, kila akipita wa mwisho wao anarejeshwa wa mwanzo wao, Na ataendelea kuwa katika hali hii ya adhabu kwa muda wote wa siku ya Kiyama ambayo kiasi chake ni miaka elfu hamsini, mpaka Mwenyezi Mungu atakapohukumu baina ya viumbe, na hapo atakuwa miongoni mwa watu wa peponi au watu wa motoni Ya nne: Mfugaji wa Farasi, naye ana aina tatu: Aina ya kwanza: Ni farasi ambao ni mzigo, nao ni wale ambao mtu kawafuga kwa lengo la kutaka kuonekana kwa watu, na kujifaharisha na kwa lengo la kuwapiga vita waislamu. Aina ya pili: Ambao kwake ni stara, nao ni wale ambao mtu kawaandaa kwa ajili ya kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kisha akawapa matunzo, akasimamia malisho yake na mahitaji yake mengine, ikiwemo kuyaachia madume haki yake. Aina ya tatu: Ambao kwake ni malipo, nao ni wale ambao mtu kawafuga kwa ajili ya kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya waislamu, akawaweka katika uwanja wa malisho kwa ajili ya chakula, hakuna watakachokula hapo isipokuwa ataandikiwa mema kwa idadi ya kile walichokula, na ataandikiwa mema kwa kila kinyesi chao na mikojo yao, na wala hawatokata kamba yao wanayofungwa nayo, wakakimbia na kutimka mbio katika maeneo yenye miinuko katika Ardhi, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamuandikia mema kwa kila athari (alama) ya unyayo na kinyesi chao, na wala mmiliki wake hatowapitisha katika mto wakanywa katika mto huo, hata kama hakukusudia kuwanywesha isipokuwa Mwenyezi Mungu atamuandikia mema kwa idadi ya fundo walizokunywa. Kisha akaulizwa rehema na amani ziwe juu yake kuhusu punda wa mjini je naye mtu atampatia malipo mfano wa farasi? Akasema kuwa: Haijateremshwa sheria yoyote kuhusu hilo isipokuwa aya hizi chache kimtazamo, ambazo zinakusanya kila aina ya ibada na maasi; nayo ni kauli yake Mtukufu: "Basi yeyote atakayefanya uzito wa chembe ndogo jema basi ataliona, na yeyote atakayefanya uzani wa chembe ndogo jambo baya basi ataliona". [Azzalza: 8], atakayefanya jambo jema katika ufugaji wa punda basi naye thawabu za hilo ataziona, na endapo atafanya maasi basi ataiona adhabu yake, na hii inajumuisha amali zote.

فوائد الحديث

Uwajibu wa kutoa zaka, na ahadi ya adhabu kali kwa mwenye kuzuia.

Hakufuru mtu aliyezuia kutoa zaka kwa uzembe, lakini yupo katika hatari kubwa.

Mwanadamu hulipwa kwa kila kipengele kinachotokea katika ibada, endapo atakusudia kupata malipo toka mwanzo wa kitu, hata kama hatokusudia mchanganuo huo.

Katika mali kuna haki zingine nje ya zaka.

Miongoni mwa haki katika ngamia ni kumkamulia maziwa anayehudhuria wakati wa manywesho yao katika masikini; ili kumrahisishia muhitaji kupata nguvu ya kufika nyumbani, na nikuwapunguzia mzigo wanyama, anasema bin Battwal: Katika mali kuna haki mbili: Faradhi ya lazima, na faradhi ya kujitosheleza, kuwakamulia watu maziwa ni katika haki ambazo huhesabika ni katika tabia njema.

Miongoni mwa haki za wajibu katika ngamia na ng'ombe ni kuliachia dume endapo litahitaji kupanda.

Hukumu ya punda na vyote ambavyo havikutajwa katika sheria nikuwa: Vyote vinaingia ndani ya kauli yake Mtukufu: "Yeyote atakayefanya uzito wa chembe ndogo jambo jema basi ataliona, na atakayefanya uzito wa chembe ndogo ya jambo baya basi ataliona".

Aya inahamasisha katika kufanya heri japo ndogo, na inahofisha kufanya shari hata ikiwa yakudharauliwa.

التصنيفات

Maisha ya Akhera., Wajibu wa Zakkah na Hukumu ya Mwenye kuiwacha., Waq'fu.