إعدادات العرض
Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amefaradhisha faradhi basi msizipoteze, na akaweka mipaka basi msiivuke, na akaharamisha vitu basi msivivamie, na akayanyamazia mambo kwa kukuhurumieni si kwa kusahau basi msiyatafute
Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amefaradhisha faradhi basi msizipoteze, na akaweka mipaka basi msiivuke, na akaharamisha vitu basi msivivamie, na akayanyamazia mambo kwa kukuhurumieni si kwa kusahau basi msiyatafute
Kutoka kwa Abuu Tha'laba Al-Khushani Jurthuum bin Naashiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amefaradhisha faradhi basi msizipoteze, na akaweka mipaka basi msiivuke, na akaharamisha vitu basi msivivamie, na akayanyamazia mambo kwa kukuhurumieni si kwa kusahau basi msiyatafute".
الترجمة
العربية Español አማርኛ English اردو Indonesia বাংলা Français Türkçe Русский Bosanski සිංහල हिन्दी 中文 فارسی Tiếng Việt Tagalog Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు தமிழ் မြန်မာ ไทย Deutsch پښتو অসমীয়া Shqip Nederlands ગુજરાતી Кыргызча नेपाली Lietuvių دری Српски тоҷикӣ Kinyarwanda Română Magyar Čeština Moore Malagasy Oromoo ಕನ್ನಡ Wolof Azərbaycan O‘zbek Українська ქართული Македонски ភាសាខ្មែរ Bambara ਪੰਜਾਬੀ मराठी Kirundi Kurmancî Bahasa Melayuالشرح
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu amewajibisha mambo na akafaradhisha faradhi basi shikamaneni nazo na wala msifanye uzembe katika hayo kwa kuyaacha au kuzembea ndani yake, na akakuwekeeni vizuizi na makemeo yaliyokadiriwa yanayokuzuieni na kukukemeeni katika yale asiyoyaridhia, msizidishe zaidi ya yale yaliyoamrishwa na sheria, na akaharamisha maharamisho kadhaa msiyachukue na wala msiyakaribie, na yasiyokuwa hayo kayaacha na akayanyamazia kwa kuwahurumia waja wake, hivyo yanabakia katika asili ya uhalali wake basi msiyatafute.فوائد الحديث
Hadithi ni ushahidi kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mleta sheria, hivyo amri iko mkononi mwake Yeye Mtukufu.
Hadithi imekusanya kanuni za sheria kwa kutoa hukumu na kuhalalisha, hivyo: Hukumu ya kisheria ima iwe imewachwa bila kusemwa au iwe imeelezwa wazi kwa uwajibu au sunna, na ama katazo kwa lazima au kwa hiari, au yaliyokatazwa kwa uharamu au machukizo, au halali.
Nikuwa aliyoyanyamazia Mwenyezi Mungu akawa hakuyafaradhisha, na hakuyawekea mpaka, na wala hakuyakataza, basi hayo ndio halali.
Uzuri wa ufafanuzi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kiasi ambacho ameileta hadithi kwa migawanyiko hii ya wazi.
Uwajibu wa kuhifadhi faradhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Uharamu wa kuvuka mipaka ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
التصنيفات
Adhabu.