Kaa kiasi cha siku ambazo ilikuwa ikidumu hedhi yako, kisha oga

Kaa kiasi cha siku ambazo ilikuwa ikidumu hedhi yako, kisha oga

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Hakika mama Habiba bint Jahshi aliyekuwa chini ya Abdulrahman bin Auf alilalamika kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu damu, akasema kumwambia: "Kaa kiasi cha siku ambazo ilikuwa ikidumu hedhi yako, kisha oga". Akawa akioga kila wakati wa swala.

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Alilalamika mmoja kati ya Masahaba wa kike kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuendelea kushuka kwa damu yake, Akamuamrisha aache kuswali kwa kiwango cha siku alizokuwa akikaa hedhi yake kabla ya kushuka jambo hili lililojitokeza kwa dharura, kisha aoge na aswali, akawa akioga kwa hiyari kwa kila swala.

فوائد الحديث

Damu ya ugonjwa ni: Mwanamke kuendelea kutoka damu baada ya siku za hedhi yake ya kawaida kumalizika.

Mwanamke mwenye damu ya ugonjwa (Istihadha) atajichukulia kuwa ana hedhi kwa kipindi ambacho hedhi yake ilikuwa ikimuijia, kabla hakijampata kilichompata katika damu ya ugonjwa.

Kikipita kiwango cha siku za ada yake ya asili, hapo atazingatiwa kuwa katwaharika na hedhi -hata kama damu ya ugonjwa itaendelea kutoka- ataoga josho la hedhi.

Mwenye damu ya ugonjwa (Istihadha) halazimiki kuoga kila wakati wa swala; kwa sababu kuoga kwa mama huyu -radhi za Allah ziwe juu yake- kulikuwa ni kwa jitihada zake, na lau kama ingelikuwa wajibu, angelibainisha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-.

Mwenye damu ya ugonjwa analazimika kutawadha kila wakati wa swala; kwa sababu kutengukwa kwake udhu ni endelevu hakukatiki, na mfano wa mwanamke huyu ni sawa na yeyote mwenye kutengukwa udhu kusikoisha, kama mwenye tatizo la kutojizuia na mkojo, au kutokwa na upepo endelevu.

Kuwauliza wenye elimu yale yenye kutatiza katika mambo ya dini, kiasi kwamba mwanamke huyu alilalamika kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-, na akamuuliza kuhusu kuzidi kwa damu inayomtokea.

التصنيفات

Hedhi Nifasi na Damu ya Ugonjwa.