Atakayevaa hariri duniani hatoivaa Akhera

Atakayevaa hariri duniani hatoivaa Akhera

Imepokelewa kutoka kwa Omari radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayevaa hariri duniani hatoivaa Akhera"

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwanaume yeyote atakayevaa hariri duniani hatovaa Akhera endapo hatotubia, na hii ni adhabu kwake.

فوائد الحديث

Makusudio ya hariri ni hariri halisi ya asili, ama hariri ya bandia ya viwandani haihusiki hapa katika hadithi.

Katazo la kuvaa hariri kwa wanaume.

Katazo la kuvaa hariri linahusu kuivaa na kuitandika.

Wanaume wanaruhusiwa kutumia hariri katika nguo ila isizidi kiwango cha vidole viwili mpaka vinne, itakayofanywa kama mchoro au urembo wa nguo.

التصنيفات

Adabu za kuvaa.